Nchimbi aahidi kumaliza kero ya barabara

LUDEWA : MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ameahidi neema kubwa kwa wakazi wa Ludewa baada ya kutangaza miradi mikubwa ya barabara zitakazojengwa na kuboreshwa kwa viwango bora kupitia Ilani ya CCM 2025/2030.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Dk. Nchimbi alisema ujenzi huo utaongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa na huduma huku ukiunganisha maeneo muhimu ya kiuchumi. SOMA: Rais Mwinyi : Kampeni za CCM zinaonesha taswira ya ushindi


Miongoni mwa barabara zilizotajwa ni pamoja na barabara ya  Njombe-Ludewa na Lusitu–Madilu–Lugarawa, pamoja na barabara za ndani za Ludewa mjini zitakazowekwa lami.

Dk. Nchimbi alisisitiza kuwa utekelezaji wa Ilani mpya utaendelea kujikita katika miradi ya maendeleo itakayowezesha wananchi kunufaika moja kwa moja.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… Y You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good eaning opportunity.tab for more detail thank you……..

    For details check ——-⫸ http://www.join.money63.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button