Majaliwa: Kuichagua CCM ni kuchagua Maendeleo

PEMBA, Zanzibar: MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuchagua wagombea wa chama hicho Oktoba 29, mwaka huu ni kuchagua maendeleo.
Majaliwa alisema hayo katika Viwanja vya Kwareni, Pemba Zanzibar wakati akizindua kampeni katika Jimbo la Kiwani juzi na kusema chama hicho kimejipanga kuendelea kuleta maendeleo katika sekta zote.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla anagombea uwakilishi wa jimbo hilo. Majaliwa alisema mara zote CCM imekuwa ikigusa maendeleo kwa Watanzania katika sekta zote, hivyo kuwapigia kura wagombea wake ni kuchagua maendeleo.
“Pemba ya leo, Zanzibar ya leo ni tofauti na tulipotoka. Hatua za kimaendeleo katika maeneo haya ni kubwa na yanaonekana kila sekta imeguswa. Mimi pia ni shahidi, nilifungua kituo cha afya hapa na sasaninaambiwa kinatumika na mnanufaika nacho,” alisema.
Majaliwa alitoa wito kwa Wazanzibari wachague wagombea urais waTanzania na Zanzibar kupitia CCM kwa kuwa wameonesha wanaweza kusimamia maendeleo katika maeneo yao. “Rais Samia na Dk Mwinyi nimadaktari wa maendeleo, hawa wote ni wasikivu, waadilifu, waaminifu na wapenda maendeleo. Wachagueni viongozi hawa ili wafanye kazi nanyi.
Hawa ni wapenda maendeleo namba moja, wanasikiliza kero na kuzifanyia kazi,” alisema. Kwa upande wake, Abdulla aliahidi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa uaminifu na ndani ya miaka mitano atazitatua changamoto Chilombe alitoa shukrani hizo wilayani Tunduru jana kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kumuombea kura Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,
Samia Suluhu Hassan. Ameishukuru CCM kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama kugombea katika Jimbo la Tunduru Kusini. Chilombe alisema kutokana na imani ya Rais Samia kwa wananchi wa Tunduru, kura zote za wananchi hao watamzawadia mgombea urais, wagombea ubunge na wagombea udiwani wa CCM.
Akitoa sera na ahadi kwa wananchi, Chilombe alisema kitu kitakachosaidia wagombea wa CCM kupita kwa kishindo ni kutokana na fedha nyingi Rais Samia alizomwaga katika wilaya hiyo kwa ajili ya kukamilisha mradi mkubwa wa umeme.
Alibainisha kuwa kutokana na matumizi madogo ya umeme unaofika megawati nne, mradi huo utasaidiaWilaya ya Tunduru kuwa na nyongeza ya umeme kwa sababu utazalisha megawati 120. “Mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 150 umeleta maajabu katika Wilaya ya Tunduru.
Kama kuna watu wanataka kuona maajabu, waje Tunduru. Tunduru inaenda kuwa na umeme wa ziada wa megawati 116 kwa sababu sisi Tunduru tunatumia megawati nne,” alisema Chilombe. SOMA: SGR Uvinza-Musongati, funguo muhimu milango mipya ya uchumi
Wakati huo huo mgombea ubunge katikaJimbo la Tunduru Kaskazini, Sikudhani Chikambo pia alimshukuru Rais Samia kwa kutatua changamoto kubwa ya mbolea iliyokuwa ikiwatesa wananchi kwa miaka mingi.
Chikambo alitoa shukrani hizo jana wilayani Tunduru kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CCM, Samia pamoja na wabunge na madiwani wa CCM. Alisema ilifikia kipindi upatikanaji wa mbolea katika wilaya hiyo kuwa mgumu, kiasi cha wananchi kuiona bidhaa hiyo kuwa anasa na wengine kukata tamaa kuitumia.
Aliongeza kuwa, kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na serikali chini ya Rais Samia, hivi sasa wananchi wananunua mbolea watakavyo muda wowote, akitolea mfano kuwa ununuzi wa mbolea sasa umekuwa kama soda.
Mwananchi anaamua na kuchagua aina ya soda atakayo wakati wowote. “Rais umefanya makubwa katika wilaya yetu kuanzia katika sekta ya elimu, afya, maji na Barabara. Mambo ni safi ikiwa ni pamoja na kilimo, ambapo wananchi wananunua mbolea kama soda, tofauti na zamani,” aliongeza.
Kwa upande wa barabara, alisema serikali imedhamiria kuifungua Tunduru baada ya kuiweka barabara katika Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025 hadi 2030, barabara ambayo ilikuwa kikwazo ya Mlingoto – Nalasi – Mchoteka hadi Mtwara Pachane yenye urefu wa kilometa 350.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, historia inaenda kuandikwa kwa kuchaguliwa mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza katika majimbo mawili ya Wilaya ya Tunduru. Aliwaahidi wananchi wa Tunduru Kaskazini kuwa wakimchagua, atahakikisha kuwa ilani ya CCM inatekelezwa kikamilifu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.



