CUF kujenga makazi bure

ARUSHA: MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Wananchi ( CUF) Gombo Samandito Gombo amesema endapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kitahakikisha katika miji ambayo ndio nguzo kuu za maendeleo inapewa kipaumbele hususani katika uboreshaji wa miundombinu ikiwemo kununua viwanja na kuwajengea wananachi makazi bure.

Gombo ameyasema hayo eneo la Kwamrombo jijini Arusha wakati wa mkutano wa hadhara ambapo alisisitiza zaidi maendeleo katika ukuzaji uchumi.

Ametaja miji itakayopewa kipaumbele kuwa ni Arusha ,Dar es salaam, Mbeya Dodoma, na Mwanza kwa sababu ya umuhimu wake huku akisema atanunua viwanja na kujenga nyumba kisha kuzigawa bure ili wananachi waweze kupata makazi .

“Miji hii ni muhimu kutokana na maendeleo kukua kwa kasi lakini pia biashara zake zinasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kupata fursa mbalimbali lakini nitawanunulia viwanja bure na kuwajengea nyumba ili mpate makazi bora.

Sambamba na hilo pia Mgombea urais huyo alibainisha kuwa endapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kihakikisha kunakuwepo na huduma bure ya uunganishaji wa umeme kwa wananchi ikiwemo kujenga nyumba na kugawa bure kwa wananachi

Naye Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Zuberi Hamisi amewaomba wananchi kumpigia kura ili aweze kuleta maendeleo kwani Jiji hilo linachangamoto mbalimbali ikiwemo kero ya maji, barabara, takataka ikiwemo ukosefu wa stendi ya kisasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button