Mashine mpya ya umeme yawasili Mtwara

MTWARA: SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Mtwara limepokea mashine kwa ajili ya kufungwa katika kituo cha umeme cha Hiari Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara ili kuongeza nguvu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia.

Hayo yamejiri wakati iliyopowasili mashine hiyo kutoka Jijini Dar es salaam na kusafirishwa kwa meli iitwayo JUZUR.ALCAMAR na kupokelewa katika Mamlaka ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoani Mtwara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, Lazaro Twange, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Irene Gowelle amesema hivi karibuni kituo hicho kulikuwa na changamoto ya mashine ya kuzalisha umeme baada ya kupata itilafu hivyo kupelekea upungufu kwenye huduma hiyo.

‘’Ujio wa mashine hii unakwenda kuongeza nguvu ya uzalishaji umeme utakaosaidia kufikia takribani megawati za uzalishaji 70 kwa ujumla hivi sasa katika mashine zilizokuwa zinafanya kazi hapa mtwara tulikuwa na uwezo wa kufikia megawati 50 lakini hii inapofungwa inakwenda kuongeza nguvu kufikia hizo megawati 70’’amesema Gowelle

Ameongeza kuwa, ‘’Mashine hii inakuja kwa lengo la kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme kutokana kwamba kipindi cha hivi karibuni tulikuwa na changamoto kidogo ya mashine yetu ambayo ilipata itilafu ya uzalishaji umeme kwa njia ya gesi asilia megawati 20 iliyoko katika kituo chetu hicho cha mtwara two’’

Amesema kufuatia uwepo wa changamoto hiyo walichukua hatua za haraka kuweza kurekebisha hali hiyo ikiwemo uletaji wa mshine hiyo kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uzalishaji umeme ili kuwezesha uhakika wa huduma.

Aidha, wamekuwa wakiwataarifu wateja pale ambapo kunatotekea upungufu wa huduma hiyo unaosababishwa na mashine ambayo ilikuwa na itilafu kwa kutokufanya kazi vizuri kupitia njia zao mbalimbali za mawasiliano ikiwemo vyombo vya habari na licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo inayafanyiwa kazi kwa sasa lakini mazingira ya upatikanaji ya umeme kwenye mikoa hiyo ni mzuri.

Pia matarajio yao baada ya kufungwa mashine hiyo kwa kiasi kikubwa ni kusaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara huku zoezi la ufungaji wa mashine  ukitarajiwa kuchukua takribani mwezi mmoja ila itategemea na watalaamu wao watakavyofanya kazi hiyo kwa haraka ili kuharakisha upatikanaji huduma.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button