ACT yataka ipewe nafasi kuharakisha miradi

KIGOMA: MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amesema ni muhimu mradi wa ujenzi wa chelezo cha kutengeneza meli katika eneo la Katabe Manispaa ya Kigoma Ujiji uharakishwe.

Zitto alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Kamara Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji. Alidai mradi huo una thamani ya zaidi ya Sh bilioni 600 na una umuhimu kwa kuwa utainua uchumi kwa kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi  wa jimbo hilo na maeneo mengine ya Mkoa wa Kigoma. “Ujenzi wa meli ukianza, karibu watu 1,000 watakuwa wanafanya kazi kila siku. Hata hivyo, maneno ni mengi ku[1] liko vitendo. Tunataka kuona utekelezaji unafanyika haraka,” alisema Zitto.

Alisema kuharakisha utekelezaji wa mradi huo anahitajika mbunge ambaye atasimama na kuipigia kelele serikali. Hivyo, aliwaomba wananchi katika jimbo hilo wampigie kura Oktoba 29, mwaka huu. SOMA: Viongozi wa CCM Kigoma wakwazwa ukarabati MV Liemba

Naye Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Taifa, Abdul Nondo alisema Mkoa wa Kigoma unahitaji wabunge wanaoweza kujenga hoja, ili miradi ipelekwe na itekelezwe Kigoma. Nondo alisema ni muhimu mkoa upate wabunge watakaoweza kusimamia fedha za miradi ili kuepuka matumizi mabaya na akaomba wananchi wamchague Zitto akasimamie hayo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button