Neema yaja wakulima wa parachichi Wanging’ombe

NJOMBE: Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi, amewahakikishia wakulima wa parachichi na mahindi wilayani Wanging’ombe kwamba serikali itakayoundwa na CCM itajenga viwanda vya kusindika na kuchakata mazao, ili kupunguza upotevu wa mazao shambani na kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumza Septemba 22, katika mkutano wa kampeni, Dk Nchimbi alisema katika miaka mitano ijayo CCM itawekeza nguvu kubwa kwenye ujenzi na uboreshaji wa viwanda, barabara, huduma za afya na elimu, huku akisisitiza kuwa kila ahadi ya chama hicho huambatana na utekelezaji.

Miongoni mwa ahadi alizozitoa ni:

Afya: Kuboresha Hospitali ya Wilaya ya Wanging’ombe kwa majengo mapya, vifaa vya kisasa na madaktari bingwa, ujenzi wa vituo vitatu vya afya na zahanati tano.

Elimu: Shule tatu mpya za msingi, madarasa 60, maabara 10 za sayansi, nyumba za walimu 20 na mabweni 25.

Miundombinu: Ujenzi wa barabara za lami ikiwemo Njombe–Iyaga (km 74), madaraja likiwamo la Kidugula na barabara za changarawe km 40.

Kilimo na maji: Visima vya maji 150, mabwawa ya umwagiliaji, mbolea ya ruzuku na huduma bora za ugani.

Umeme: Kufikisha umeme kwenye kila kijiji na kitongoji cha Wanging’ombe.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button