Museveni aidhinishwa kugombea urais

KAMPALA,Uganda : TUME ya Uchaguzi ya Uganda imemuidhinisha Rais Yoweri Museveni kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. Museveni, mwenye umri wa miaka 81, amekuwa madarakani tangu 1986 na sasa anataka muhula wa saba.

Museveni aliwasili kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi akiwa ameambatana na mkewe Janet Museveni na viongozi wakuu wa chama chake cha NRM. Katika hotuba yake ya uteuzi, alishukuru chama kwa kumpa ridhaa na kuahidi kuendeleza uchumi wa nchi hiyo.

Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambaye atateuliwa na chama chake kesho. Uchaguzi mkuu wa Uganda umepangwa kufanyika Januari 12 mwakani. SOMA: Rais Museveni kugombea tena urais

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button