Gairo yanukia utajiri wa parachichi

MOROGORO: WILAYA ya Gairo, mkoani Morogoro imeanza kuchipukia kuwa kitovu kipya cha uzalishaji wa parachichi nchini kutokana na juhudi za serikali na wadau wa kilimo kuendeleza zao hilo kwa lengo la kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.

Hatua hiyo inatokana wakulima wa vijiji vya tarafa ya Ngonwe katika wilaya hiyo kuwepo kwa mazingira mazuri ,hali ya hewa na udongo unaofaa kwa ustawishaji mkubwa zao  la parachichi.

Ofisa Kilimo wa halmashauri ya wilaya hiyo, Phillemon Issack  akizungumza na HabariLeo amesemsa kuwa  tayari miche ipatayo 105,360  ya parachichi ilishasambazwa kwa vikundi vya wakulima wa vijiji vya Tarafa ya Ngongwe.

“ Tumeweka matarajio ya kuvuna tani 460. 08  za mwanzo kwa mwaka 2028 na baada ya hapo mavuno kwa tani yataongezeka zaidi kila mwaka” amesema Phillemon.

Naye mkuu wa mkoa huo, Adam Malima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa maonesho ya “Samia Kilimo Biashara Expo 2025 Gairo”, msimu wa nne, yatakayofanyika kuanzia Septemba 28,mwaka huu wilayani humo  amewataka   wakulima kuwa na mawazo mapya na kuachana na kilimo cha mazoea ambacho mara nyingi hakileti tija kubwa.

Amesema maonesho hayo ni fursa adhimu kwa wakulima wa mkoa huo na mingine ya jirani na kwamba wananchi watajifunza ili kuboresha maarifa na uhusiano wao na wadau wa maendeleo ya sekta aya kilimo.

“Mwaka huu ni msimu wa nne wa Samia Kilimo Biashara Expo na unaweka msisitizo mkubwa katika kuunganisha wakulima na taasisi za kifedha, watafiti, na wawekezaji, tunawataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwa kuwa fursa hii haiwezi kupatikana kila siku,” amesema Malima.

Malima amesema maonesho hayo yanatarajiwa kuzinduliwa Septemba  28, mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabir  Makame, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo miaka minne iliyopita.

“Ushiriki wake unachukuliwa kama ishara ya heshima kwa mchango aliowahi kutoa katika kukuza sekta ya kilimo katika wilaya hiyo hususani zao la Parachichi” amesema  Malima.

Mkuu huyo wa mkoa amesema Serikali ya mkoa pamoja na Wilaya hiyo wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi kuwa kila zao linaweza kuwa zao la biashara endapo tu litazalishwa kwa wingi ama zaidi ya mahitaji ya chakula na hivyo  kuondokana na kilimo chakula pekee.

Malima amesema maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2025  yatafungwa na mkuu wa Mkoa nwa Morogoro Oktoba 4, mwaka huu  katika Kata ya Rubeho.

Kwa  upande wake  Mkuu wa Wilaya hiyo , Japhari Kubecha amesema kuwa wilaya imejipanga zaidi kuhamasisha kilimo biashara kwa lengo la kuwawezesha  wakulima kuondokana na kilimo cha chakula pekee ili kuongeza uchumi kwa wakulima, halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Kubecha amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wananachi kupatiwa elimu ya kilimo biashara hususan matumizi ya  mbinu za kisasa za uzalishaji, matumizi ya teknolojia, usindikaji wa mazao,na kujenga mitandao ya kibiashara.

Habari Zifananazo

6 Comments

  1. ……………. Atembelea chuo chake alichosoma bila nguo wenzake waamua kumpatia nguo ambazo hazistahili matako

  2. Akutana na kiongozi wake na kumwambia “Mwanao na wewe Ndio mnatakiwa kutuletea aina ya umalaya mathalani………….

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button