Tehama yapaisha usajili watahiniwa PSPTB

MOROGORO: BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imesema matumizi ya mifumo ya Tehama imeleta mafanikio makubwa katika usajili  wakitaaluma na kufikia wanataaluma zaidi ya 11,000 ikiwa na idadi kubwa ya wanaojisajili kufanya Mitihani ya taaluma ya Bodi kwa mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji, Godfred  Mbanyi amesema hayo kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika  mjini Morogoro

Mbanyi amesema  baraza la wafanyakazi lililokuwa na jukumu la kupitia tathimini  ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo ilifungwa Juni 30 mwaka huu ili  kuangalia yaleyaliyopangwa kufanyika , walipofanya vizuri na walipokwama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo amesema kuwa Bodi imepata mafanikio makubwa  kwenye usajili wa kitaaluma ambapo hadi sasa wapo zaidi ya 11,000 ambao wamejasiliwa kwa kutumia mifumo ya Tehama .

Amesema  kwa upande wa  Mitihani ya taaluma ya Bodi hufanywa mara mbili kila mwaka yaani, Mei na Novemba  na kwa kutumia Tehama  idadi imekuwa ni ya kuridhisha kwa sababu kwa mwaka jana (2024) lengo lilikuwa ni watahimiwa 750 na waliweza kufikia 680 ambao ni wastani mzuri.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa kilichowezasababisha ongezeko hilo , ni urahisi wa kuwafikia wadau wao  kutokana na  Bodi kuwekeza kwenye  matumizi ya mifumo ya Tehama.

“ Sasa hivi tunatumia mifumo ya Tehama  tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo watahiniwa au wanaoomba usajiri wa kitaalamu walikuwa wanalazimika kwenda kulipia ada ya uanachama au  ada ya  maaombi kwa kwenda kupanga foleni Benki” amesema Mbanyi.

“ …Hivi mtu anaingia kwenye mfumo mwenyewe anajaza form ana click anapata control number mwenyewe huko aliko analipia kule kule kwa kutumia simu kwa hiyo inakuwa ni kitu ambacho ni rahisi ndio maana unaona namba inazidi kupanda na tunatarajia  kwa mwaka unaokuja wa fedha tutakuwa nafasi nzuri zaidi” amesema .

Mbanyi ametoa  rai kwa wadau, wanunuzi wa ugavi , wazazi , watahiniwa na wataalamu waendelee kushirikiana na bodi hiyo ikiwa na kujiandikisha kwa ajili ya mitihani , ujisajiri wa kitaaluma na wanaodaiwa ada za uanachama waendelee kulipa.

Naye Katibu wa Tughe Tawi ya PSPTB, Faraja Mgulambwa ameupongeza  uongozi wa Bodi hiyo kwa  kuwezesha kufanikisha baraza hilo ambalo ni muhimu na linaloweka tija katika taasisi.

“ Wafanyakazi wanakuwa huru , umoja na kuwasilisha mambo mbalimbali yanayoleta tija katika taasisi na baraza hili ndilo kufanikisha malengo ya taasisi kwa wadau wetu wa ununuzi na ugavi” amesema  Faraja.

Kwa upande wake Mtumishi wa Bodi hiyo Nancy Mwamakimbula amesema  wafanyakazi wananufaika na mabaraza hayo kwa vile ni  sehemu pekee ambapo wajumbe wote wako sawa kwa maana ya menejimenti ,viongozi na watumishi wa kawaida  kutoa mawazo mchango wao na maoni yao kwa uhuru na  kusikilizwa.

“Sisi wajumbe tunatoa maoni yetu yanapokelewa na yanafanyiwa kazi kama kuna changamoto pia tunazieleza zinasikilizwa, zinachukuliwa na kutekelezwa na kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za kiutumishi na  lengo letu kubwa ni kwa ajili ya kuboresha” amesema Nancy.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button