MSD yafikia 80% usambazaji vifaa tiba, dawa

TANGA: Bohari ya dawa imeweza kuboresha upatikanaji wa huduma ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya kutoka asilimia 50 hadi kufikia asilimia 80 katika kipindi cha mwaka 2024/25.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Kanda ya Tanga, Grant Mwapwele wakati wa ufunguzi wa kikaow cha wateja na wadau wa Bohari ya Dawa Kanda ya Tanga ambapo amesema kuwa maboresho hayo yamesaidia vituo vya afya kuwa na vifaa tiba vya kisasa .
Amesema kuwa kwa upande wa kanda ya Tanga yenye jumla ya vituo vya afya 568 wameweza kusambaza dawa zenye thamani ya Sh bil 22.5 katika kipindi cha mwaka 2024/25.
“Licha ya mafanikio hayo lakini kumekuwa na changamoto ya malimbikizo ya madeni kutoka kwenye vituo hivyo na kuwaomba wasimamia kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa wakati,”amesema Mwapwele.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, William Mwakilema amewataka wasimamizi wa vituo vya afya kudhibiti usimamizi wa fedha ili kupunguza madeni kutoka Bohari ya Dawa MSD lakini na wananchi wakiendelea kupata huduma bora za afya ikiwemo dawa na vifaa tiba
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Cash43.Com