Mgombea ubunge Ngorongoro ampa sifa Dk Samia

ARUSHA: MGOMBEA ubunge Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Yannick Ndoinyo amesema kuwa Rais wa kwanza nchini tangu uhuru kuwasikiliza viongozi wa Kimilla wa Jamii ya Kifugaji ya Kimasai Ngorongoro ni Rais Samia Suluhu Hassan na alijadiliana nao changamoto za uhifadhi na ardhi katika jimbo hilo na kuzitatua mara moja.

“Rais Samia ndiye Rais wa kwanza toka Tanzania ipate uhuru kuwasikiliza viongozi wa kimila maarufu kwa jina la Malaiguanani zaidi ya 150 na hiyo imetupa faraja kubwa sana ni Mama msikivu,mnyenyekezo na mcha Mungu na tayari ameshatutatulia changamoto zilizokuwa zinatukabili na ninawaomba wananchi wa Ngorongoro tumchague awe Rais wetu,” amesema Ndoinyo.

Ndoinyo alitoa kauli hiyo wakati wa mikutano yake ya kampeni katika Tarafa ya Ngorongoro na na kusisitiza kuwa wananchi wa Ngorongoro wanapaswa kuendelea kuiamini CCM kwa kazi kubwa zinazotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia.

Alisema kila mmoja ifikapo octoba 29 mwaka huu ahakikishe anakwenda kupiga kura ya Rais ili aweze kuleta nchi maendeleo zaidi katika Jimbo hilo na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni mgombea pekee mwenye kusikiliza kero na kuzipata majawabu hapo hapo.

Miongoni mwa wakazi wa kata za tarafa ya Ngorongoro aliyejitambulisha kwa jina la,Nanyai Sungare,mkazi wa kata ya Olbalbal na Elius Ngorisa,mkazi wa kata ya Ngoile pia walieleza imani yao kwa Rais Samia na wagombea wa CCM na kusema kuwa siku ya kupiga kura ikifika watawapigia wagombea wote wa chama tawala akiwemo Rais,ubunge na udiwani.

“Tunamwamini Mama Samia na wagombea wa CCM kwa sababu wamesikiliza kilio chetu.”Alisema Sungare

“Hii ni mara ya kwanza tunaona Rais anashirikiana na viongozi wetu wa kimila. Tunachagua CCM kwa maendeleo.”Alisema Ngorisa

Wilaya ya Ngorongoro, yenye kata 28, inatarajia kuwa na wapiga kura zaidi ya 170,000 kwenye uchaguzi huu, ambapo wananchi wengi wameonyesha dhamira ya kuiunga mkono CCM kuanzia ngazi ya Rais, mbunge hadi madiwani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button