Samia amefanya makubwa Pwani

PWANI : MBUNGE mteule wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Chakoma amemsifu mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza makusanyo ya mapato kutoka Sh trilioni 18 hadi kufi kia trilioni 32 ndani ya miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Chakoma alieleza hayo wakati akimuombea kura Samia kupitia mkutano wa kampeni uliofanyika Kibaha mkoani Pwani jana. Aalisema kutokana na miongozo na maelekezo ya mgombea wao makusanyo ya mapato katika Halmashauri ya Chalinze na Kibaha mkoani humo. “Miongozo na maelekezo ya Rais Samia yakatushukia Mkoa wa Pwani, jambo ambalo limefanya mkoa wetu kurithi kutoka kwako kwa kuongeza makusanyo.

“Halmashauri ya Chalinze wakati unaingia 2021 walikuwa wanakusanya bilioni tisa (Shilingi) lakini miaka yako minne Chalinze inakusanya bilioni 22, katika Halmashauri ya Kibaha wakati unaingia makusanyo yalikuwa Shilingi bilioni mbili lakini miaka yako minne mgombea makusanyo yameenda mpaka bilioni 10,” alisema. Chakoma alisema kupitia fedha za makusanyo hayo Mkoa wa Pwani umefanikiwa kupata miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, zahanati, miradi ya maji, elimu na miundombinu.

Alimshukuru mgombea wa chama hicho kwa uwekezaji uliofanyika katik Kongani ya Kwala iliyoongeza mapato ya mkoa huo. Sambamba na mafanikio katika ukusanyaji wa mapato Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha wananchi wa Mkoa wa Pwani kupata Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi ya Bibi Titi Mohamed iliyojengwa Rufiji kwa gharama ya Sh bilioni 4.4.

Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini wa chama hicho, Hamoud Jumaa alisema ana imani kuwa CCM itapata ushindi wa kishindo kutokana na kazi nzuri zilizofanywa katika miaka minne ya Serikali ya Awamu wa Sita. Alisema katika miaka hiyo minne, Kibaha Vijijini imepokea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika elimu, maji, afya, umeme na miundombinu Jumaa alisema mgombea huyo ameboresha bandari na kuongeza kiwango cha mizingo kufikia tani 32 kutoka tani 18.

Alisema mgombea huyo amewezesha vijiji 8,500 kuunganishwa na nishati ya umeme na kutoa Sh bilioni sita za ujenzi wa jengo la halmashauri na nyumba za watumishi. Pia, katika elimu Serikali ya Awamu ya Sita imepeleka Sh bilioni 1.2 kwenye maendeleo ya shule za msingi na Sh bilioni 3.5 kwa ajili ya shule za sekondari “Sisi tunakushukuru kwa fedha za miradi ya maendeleo…

Kwenye elimu umetuletea bilioni moja na milioni 289 (Shilingi) kwa ajili ya shule za msingi; tumejenga shule tatu na madarasa 61, sasa tuna madarasa 416,” alisema. Alisema kupitia mapato ya halmashauri wananchi wa Kibaha Vijijini wamenufaika na Sh bilioni moja za mikopo ya halmashauri. SOMA: Migiro, Kikwete waeleza sababu CCM kuchaguliwa

Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Bagamoyo kwa tiketi ya CCM, Subira Mgalu alisema jimbo hilo limepokea Sh bilioni 27 za miradi ya maendeleo iliyofanya mapinduzi katika sekta ya afya, elimu, maji na miundombinu Alisema katika elimu Sh bilioni 15 zimetumika katika kuboresha shule za msingi na sekondari kwa kujenga shule nane za msingi na tano za sekondari pamoja na mabweni Kwa upande wa afya, Wilaya ya Bagamoyo imenufaika na Sh bilioni nne ndani ya Awamu ya Sita zilizowezesha kuboresha Hospital ya Wilaya na kujenga jengo la dharura na kumaliza tatizo la vifo vya wajawazito.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button