Mradi wa gesi Kinyerezi–Chalinze kujengwa

PWANI : MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga mtandao wa gesi kutoka Kinyerezi hadi Chalinze kuwezesha uzalishaji maeneo ya uwekezaji. Samia aliyasema hayo jana kwenye Uwanja wa Sabasaba Kibaha Mjini alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni.

“Pamoja na hayo mkitupa ridhaa tunajipanga tujenge mtandao wa gesi kutoka Kinyerezi kwenda Chalinze ambao utakuwa na matoleo kuelekea kwenye maeneo ya uwekezaji ya Tamco, Zegereni, Kwala na Bagamoyo.

Kwa sasa mkandarasi mshauri anaendelea na tathmini ya njia ya kupitisha bomba la gesi,” alisema Samia akiomba kura. Alisema ujio wa gesi Pwani utazidi kuvutia uwekezaji kwani viwanda vitaendeshwa kwa gharama nafuu zaidi na bidhaa zinazozalishwa zitapungua bei.

“Miongoni mwa ahadi zetu kwenye ilani ni kuchukua hatua za kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi ili kuwezesha wananchi hususani wa kipato cha chini kujenga nyumba bora na za kisasa na kwa gharama nafuu,” alisema.Aliahisi pia kutekeleza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na eneo la kiuchumi kama wananchi wa Pwani watampa ridhaa ya kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

“Moja ya miradi ya kimkakati mkoa wa Pwani ni Bandari ya Bagamoyo, mkitupa ridhaa ya kuendelea tunakwenda kujenga bandari katika eneo la Mbegani.Bandari hii itakuwa na gati za kisasa na ndefu ambazo zitakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi ya Bandari ya Dar es Salaam, pia itaunganishwa kwa reli ya SGR (Reli ya Kisasa) kwa kipande cha kilometa 100 kutoka Bandari Kavu ya Kwala hadi ilipo Bandari ya Bagamoyo,” alisema.

Alisema bandari hiyo itajengwa sambamba na eneo la kiuchumi la hekta 9,800, litakalochochea uzalishaji na kuvutia uwekezaji wa viwanda, “tumekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi wa bandari na eneo huru la biashara tunaenda kutekeleza mradi huu kupitia kwa TPA (Mamlaka nya Bandari Tanzania), TRC (Shirika la Reli Tanzania) na sekta binafsi hususani kwenye kongani za viwanda, huko lazima tuialike sekta binafsi iingie tufanye nao kazi pamoja,” alisema.

Alisema miradi hiyo ni ya kimapinduzi na Mkoa wa Pwani kuwa kitovu cha usafirishaji nchini itaongeza fursa ya ajira na biashara kwa wananchi wa Pwani na Tanzania kwa ujumla.

“Ahadi yetu ni kusimamia na kuiendeleza miradi hii muhimu kwa maendeleo yetu na ya nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza kuwa Pwani inastahili pongezi za pekee kwa kasi kubwa ya maendeleo ya viwanda ambayo yanazalisha ajira rasmi na zisizo rasmi. SOMA: Ngajilo ahaidi kuwa sauti ya wananchi Iringa Mjini

Alisema uwekezaji unaofanyika Pwani na kote nchini umeiwezesha nchi Tanzania kupiga hatua katika mwelekeo wa kujitegemea kimapato na kibidhaa. Alisema kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa viwanda na kutofifisha ufanisi wa uzalishaji ndani ya viwanda hivyo, serikali yake imeamua kujenga vituo vya kupoza umeme Msufini-Mkuranga kwa gharama ya Sh bilioni 388.3, Zegereni Kibaha kwa Sh bilioni 54.7 na Zinga, Bagamoyo kwa gharama ya takribani Sh bilioni 120.

“Umeme unatakiwa kuwa wa uhakika na kufanya Mkoa wa Pwani kutokuwa na upungufu wa umeme na kufanya viwanda vizalishe muda wote,” alisema. Alisema mwelekeo wa serikali ni kuendeleza ujenzi wa makazi bora kwa bei nafuu na Mkoa wa Pwani umekuwa mfano katika kuibeba ajenda hiyo ya kitaifa.

Kuhusu maji, Samia alisema walipeleka mkoani hapo Sh bilioni 187.3 kwa ajili ya maji lakini anatambua kuna maeneo bado upatikanaji wa maji haujawa mzuri. Aliongeza: “Tunapoenda mbele tutakamilisha miradi mingine minne yenye thamani ya Sh bilioni 44”.

Kuhusu miundombinu ya barabara, Samia alisema anatambua uwepo wa mahitaji hususani kutokana na msongamano wa magari katika Barabara ya Morogoro kutokana na wembamba wa barabara hiyo na kuwa, “tayari usanifu unaendelea wa upanuzi wa barabara kutoka Maili Moja hadi Picha ya Ndege ili iwe na njia sita za magari na njia mbili za BRT(Barabara za Mwendokasi”.

Akiwa Chalinze, Samia alisema serikali yake imeimarisha sekta ya kilimo na Pwani inafanya vizuri kwenye mazao ya chakula na ya biashara ikiwemo korosho, hivyo wakipewa ridhaa ya kuingia tena madarakani watayaangalia zaidi mazao ya ufuta na mkonge ndani ya mkoa huo.

Akiwa Msata, Samia aliwaagiza viongozi wa serikali kufanya uhakiki wa madai ya fidia kwa wananchi ili kupisha serikali kuendelea na miradi mbalimbali. “Fidia ilikuwa Shilingi bilioni tisa, tulishalipa yote lakini yakaja madai mengine tena ya fidia ya Shilingi bilioni nne, viongozi fanyieni uhakiki ya fedha hizo ili wananchi walipwe na miradi mbalimbali ya kimkakati iendelee,” alisema.

Aidha, Samia aliwataka wananchi kujitokeza kupiga kura na kwamba wasiogope kwani hakuna tishio lolote. “Tumejipanga vizuri mno asitokee mtu kuwatisha, tokeni mkapige kura, yamewashinda wenyewe kuingia kwenye mashindano, wasiharibu,” alisema.

 

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button