CCM yajipanga kujenga viwanda kusindika matunda, viungo Muheza

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema serikali yake itajenga viwanda vya kusindika matunda na mazao ya viungo Muheza mkoani Tanga.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan alitoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Kituo cha Mabasi cha Mvuleni Kibanda, Muheza jana.

“Baada ya kufanya kazi kubwa ya kuweka umeme Muheza kuhakikisha haukatiki katiki, tukimaliza hiyo tuna jukumu la kuweka kongani za viwanda kila wilaya na kwa Muheza hapa tutakuja na viwanda vya kuongeza thamani kusindika matunda na mazao ya viungo, ndio mazao ambayo tunaona Muheza yanalimwa kwa wingi,” alisema Samia.

Pia, alisema serikali yake itafufua viwanda vya chai Muheza.

Samia alisema kwa Muheza, masuala ya afya, elimu, maji na umeme wanaendelea kuyafanyia kazi mpaka wahakikishe kila mtoto wa Tanzania anakwenda shule kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo.

“Mpaka tuhakikishe kila Mtanzania ana huduma bora ya afya kuanzia kijijini hadi rufaa, nia yetu ni kuona kila Mtanzania yupo karibu na maji safi na salama, nia yetu kuona umeme unamuangaza kila Mtanzania,” alisema.

Kuhusu Barabara ya Muheza-Pangani na Muheza-Amani, Samia alisema ameziona hali zake, hivyo aachiwe atazifanyia kazi.

“Wakati natoka Pangani nimekuja na Barabara ya Muheza-Pangani au unaweza sema Barabara ya Pangani-Muheza, nimeiona hali yake, ina kilometa karibu 45… Nimekuta vijilami kidogo, sasa niachieni nikaifanyieni kazi,” alisema.

Aliongeza: “Vilevile, kama alivyosema Mbunge (Hamisi Mwinjuma mgombea wa Muheza), kuna Barabara ya Muheza-Amani ambayo tumeianza kama kilometa 10 hivi, ni ya kilometa 40 hivi, hiyo nayo niachieni nikaifanyie kazi”.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button