Usawa wa kikodi na mageuzi ya kiuchumi Tanzania

USAWA wa kikodi ni msingi muhimu wa haki ya kiuchumi na maendeleo jumuishi unaotenda haki kuwezesha serikali kukusanya mapato bila kubebesha wananchi wa kipato cha chini mzigo mkubwa huku ukichochea ukuaji wa sekta binafsi na uwekezaji.

Katika historia ya kodi Tanzania, enzi za ukoloni kodi zilitumika kama chombo cha udhibiti badala ya maendeleo huku kodi ya kichwa ikilazimisha wazawa kuingia kwenye uchumi wa fedha wa kikoloni. Baada ya ukoloni, Tanzania ilijaribu kujenga mfumo wa kodi wa kijamaa uliolenga kugharamia huduma za jamii kama elimu, afya na miundombinu.

Kimsingi kumekuwa na changamoto za usawa wa kikodi pamoja na ukosefu wa ufanisi katika ukusanyaji na usimamizi wake. Aidha, kumekuwapo mianya ya kukwepa kodi kwa baadhi ya kampuni kubwa huku wananchi wa kawaida wakilazimika kulipa kwa uaminifu.

SOMA: Mapendekezo mabadiliko ya kodi kuwezesha biashara

Kwa kutambua hayo, Mradi wa Usawa wa Kikodi unawezesha utoaji wa mafunzo ya masuala ya usawa wa kikodi kwa viongozi wa vikundi vya wanawake, vijana na wakulima wadogo vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.

Unalenga kuwezesha wananchi wa vijiji vya Kata ya Tomondo kutambua umuhimu wa masuala ya kikodi kwa ajili ya maendeleo, kutambua changamoto za kikodi na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Ofisa Programu Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa PELUM Tanzania, Anna Marwa.

Ofisa Programu, Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa Shirika la Participatory Ecological Land Use Management (PELUM) Tanzania, Anna Marwa anasema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2024 katika vijiji vinne vya Kikundi, Vuleni, Lukonde na Kungwe katika Kata ya Tomondo.

Anasema mradi upo chini ya usimamizi na uendeshaji wa Pelum-Tanzania na Policy Forum kwa ufadhili wa International Budget Partnership (IBP) na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD).

Kwa mujibu wa Anna, mradi unalenga kuangalia sera na sheria mbalimbali za kikodi ambazo ni rafiki na zinawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika ulipaji kodi.

Anasema Mradi wa Usawa wa Kikodi kwa wakulima unalenga kuwezesha wakulima wadogo katika masuala ya kodi na kusaidia kuwepo sheria na miongozo rafiki inayowezesha wakulima kushiriki ulipoaji kodi na usimamizi wa fedha zinazowekwa kwenye miradi inayowanufaisha kimaendeleo.

“Nchi haiwezi kuendelea bila kodi; ulipaji wa kodi ni uzalendo, kwa hiyo kama nchi inataka kuwa na mapato, wananchi wake wanapaswa kuwa na uzalendo hasa katika ulipaji kodi,” anasema Anna. Anna anasema wananchi wanapaswa kuelewa wanavyoweza kusimamia mapato katika shughuli mbalimbali za maendeleo, kusiwe na ubadhilifu wala upotevu wa fedha.

“Tunaamini wananchi wanapaswa kusimamia vizuri fedha za miradi zinazoletwa kwao vijijini hata maendeleo yaliyopaswa kuletwa kutokana na fedha ambazo zimewekezwa zinaweza kuwanufaisha wananchi wenyewe,” anasema Anna.

Kuhusu changamoto, anasema tangu walipoanza kutekeleza mradi huo wamebaini changamoto mbalimbali kwa wakulima wadogo, wanawake na vijana kuwa ni pamoja na hasa kukosa uelewa wa masuala muhimu ya kodi. Anasema changamoto ni kwamba mifumo ya ukusanyaji kodi haijawafika ipasavyo kwa wananchi vijijini na wana uelewa mdogo katika masuala ya kodi, ukusanyaji kodi na sheria za kodi.

Anasema katika maeneo kadhaa wananchi hawakuwa na nguvu ya kusimamia mapato yanayoletwa katika vijiji kwa ajili ya maendeleo. Ofisa huyo anasema kupitia Mradi wa Usawa wa Kikodi, wananchi wa vijiji hivyo wamejengewa uwezo katika masuala ya usawa wa kikodi hususani wanawake na vijana.

Kupitia mradi huo, wamesaidiwa kutambua namna wanavyoweza kushiriki sawia katika ulipaji kodi hususani wakulima. “Tunajua kuna kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na wao wanashiriki katika ulipaji kodi kwa kununua bidhaa,” anasema Anna.

Anawahimiza kuhakikisha wanalipa hata kodi nyingine ambazo wakulima wanatakiwa kulipa na si VAT pekee. Anna anasema kupitia mradi huo wanahamasisha uwepo wa sheria rafiki ambazo zitakazosaidia wakulima kuona wajibu wao kulipa kodi bila kuwa na mzigo mkubwa unaowafanya washindwe.

“Tunapozungumzia usawa wa kikodi, kuwe na sawa wa unachokilipa kulingana na mapato unayopata kama mkulima,” anasema.

Kwa mujibu wa Anna, Mradi wa Usawa wa Kikodi unalenga kuwafikia wanawake asilimia 60 kutokana na idadi yao kuwa kubwa na ni walipaji wazuri wa kodi hususani VAT kwa vile ni wanunuzi wakubwa wa bidhaa za aina mbalimbali kila siku, wakati wanaume watakaofikiwa ni asilimia 40.

Anasisitiza ulipaji kodi akisem ni jambo muhimu ili kuwezesha taifa kujitegemea kwa kuwa yanahitajika mapato zaidi kuboresha huduma za jamii zikiwemo za afya, elimu na miundombinu. “Lazima tuwe wazalendo kwa kuhakikisha tunatoa elimu ya usawa wa kikodi ili wigo la ukusanyaji kodi uongezeke,” anasema.

Kwa upande wake, Ofisa Programu na Uchambuzi wa Sera wa Policy Rorum, Samwely Mkwatwa anasema wananchi hususani wakulima, wanaelewa umuhimu wa kodi katika maisha.

Samwely anasema wananchi wanapolipa kodi, serikali nayo hupaswa kuwajibika kwao ili wananchi waone kodi inayokusanywa inakuwa msaada na manufaa kwa kujibu changamoto za kijamii wanazokutana nazo katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya vijijini.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukonde katika Kata ya Tomondo, Morogoro, Ismail Ahmadi anapongeza serikali kwa kutoa Sh milioni 528 kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya kisasa ya bweni katika kijiji hicho akisema utaondoa adha kwa watoto kijijini hapo na vijiji jirani.

Awali, watoto hao wanaosoma katika Shule ya Sekondari Tomondo walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 14 na wengine zaidi ya kilometa 15 kwe Shule ya Sekondari Mikese.

Anasema hayo katika mkutano kijijini hapo uliowashirikisha viongozi wa vikundi vya wanawake, vijana na wakulima wadogo kuhusu masuala ya kikodi kwa maendeleo, kutambua changamoto na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

“Shule hii ya kisasa ipo katika hatua ya kukamilishwa ikiwa na mabweni ya wasichana na wavulana. Ikikamilika, watoto wetu watanufaika kwa kuondokana na kutembea umbali mrefu kwenda shule za jirani,” anasema Ismail.

Anasema shule hiyo inajengwa kutokana na fedha za kodi za Watanzania wanazotoa kwa serikali yao zinazorejeshwa kwao kwa njia ya maendeleo ya kijamii.

“Ulipaji wa kodi ni jambo muhimu kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi na miongoni mwa faida hizi ni kijiji chetu; tumeletewa Shilingi milioni 528 kujenga shule ya sekondari ambayo hadi kufikia Januari 2026 itawanufaisha watoto wetu,” anasema Ismail.

Wananchi wengine wa Kijiji cha Kungwe, Kata ya Tomondo wanaeleza namna kodi inavyochangia maendeleo yao. Miongoni mwa faida hizo ni katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kutoa Sh milioni 11 kupaua jengo la madarasa mawili yaliyoezuliwa na upepo Novemba 2024.

Kwa nyakati tofauti, mkazi wa kijiji hicho, Ng’ole Mwezi ambaye ni mwanachama wa Kikundi cha Upendo pamoja na Christina Titile wa Kikundi cha Mapitio wanasema licha ya kutoa fedha hizo, uongozi wa halmashauri hiyo uchukue hatua za haraka kupaua jengo hilo.

“Wananchi wa Kungwe tunaomba halmashauri ilifuatilie kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha madarasa haya mawili yaliyoezuliwa na upepo yanakamilishwa, kuezekwa ili yahudumie wanafunzi,” anasema Mwezi. Aidha, anaomba elimu kuhusu masuala ya kodi iwekewe mkazo kwa kutolewa kwa wananchi wote wakiwamo wa vijijini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button