Ikongosi yatikisa uzinduzi wa kampeni

IRINGA: Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Ikongosi umezinduliwa kwa shamrashamra, huku mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Negro Lusani Sanga, akiahidi kuwa siku ya kupiga kura, Oktoba 29, hakuna atakayebaki nyumbani.
Sanga alisema hata wagonjwa wataamshwa, kubebwa na kupelekwa kituoni kuhakikisha kura ya ushindi wa kishindo inamwangukia Rais Dk Samia Suluhu Hassan, mbunge na diwani wa CCM.
Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi wa Ikongosi, Sanga alisema:
“Ikongosi ina wasomi na wafanyabiashara wakubwa, lakini mmempa imani mtoto wa mzee Lusani aliyekuwa na mashine ya kusaga tu. Najua ni kosa kubwa kujisifu kwa mafanikio bila kushukuru, ndiyo maana leo nipo mbele yenu kuomba tena kura zenu kwa heshima na unyenyekevu.”
Sanga alieleza kuwa kata hiyo imepiga hatua kubwa tangu mwaka 2015 hadi sasa, ikiwemo ongezeko la shule za sekondari na msingi, pamoja na ujenzi wa zahanati mpya katika vijiji mbalimbali.
Alisema pia kuwa miundombinu ya barabara imeimarika kwa kilomita tano za lami kuingia Ikongosi, lakini bado kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya barabara za vijiji vya kata hiyo.
“Awamu inayofuata itakuwa ya kuboresha barabara kwa kiwango cha juu ili mazao ya misitu na chakula yasafirishwe kwa urahisi. Tutahakikisha pia barabara ya Mafinga–Mgololo inajengwa kwa lami.”
Sanga alikemea kero ya ushuru usiokuwa na utaratibu, akiahidi kupigania haki ya wafanyabiashara na wananchi.
Kuhusu ajira na uchumi wa wananchi, Sanga alisema atasimamia utekelezaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu, huku akiahidi kuishauri serikali kuja na mpango maalumu kwa wazee.
“Wazee nao wapewe fursa ya kupewa mifugo kama nguruwe, ili wakiendeleza mifugo hiyo wanufaike pamoja na familia zao.”
Mke wa mgombea huyo, Matilda Yasin alishiriki kumpigia kampeni mumewe kwa kuwakumbusha wananchi kuwa ahadi alizozitoa mwaka 2015 zimeanza kuonekana, na kwamba ipo mipango mipya ya maendeleo itakayotekelezwa ndani ya miaka mitano inayokuja.
Aidha, mtoto wa Sanga Irine Sanga alimuombea kura baba yake, akisisitiza kuwa ni kiongozi mwenye nguvu, uwezo na maarifa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Ikongosi.
Kwa upande wake, Magreth Kaguo, diwani mteule wa viti maalumu kata ya Ikongosi, aliwataka wananchi kuhakikisha Oktoba 29 wanapiga kura tatu — rais, mbunge na diwani wa CCM — akisema:
“Mafiga mawili hayaovishi chakula. Kura tatu ndizo zitakazotuletea ushindi wa kweli.”
Alitumia jukwaa hilo kuonya dhidi ya vurugu na maandamano yanayotangazwa na baadhi ya wapinzani, akisisitiza kuwa CCM ndiyo nguzo ya amani nchini.
. Medical debt had me stressed, but this online approach has been a blessing. I now earn about $7,700 monthly. Details >>>> https://dailycash21.blogspot.com/
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com