NRA yaahidi kudhibiti upotevu mapato

DODOMA: MGOMBEA Urais kupitia chama cha NRA, Almas Hassan, amesema endapo kama watanzania watampa ridhaa ya kuongoza nchi, atajitahidi kuzuia mapato ya serikali yasipotee kwa kutengeneza namba moja ya malipo ‘control number’ itakayotumika kulipa malipo yote ya serikali.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Daily News Digital, Almas amesema kuwepo kwa chombo kimoja cha ukusanyaji kodi kutasaidia serikali kuwa na uhakika wa mapato na kumtambua kwa urahisi mtu wa kuwajibishwa endapo kutatokea upotevu wa fedha.

Amesema kwa sasa vyombo vya kukusanya kodi ni zaidi ya vitatu, vikiwemo Halmashauri, Maliasili na TRA, hali inayosababisha mkanganyiko na kutokuwa na uwazi juu ya mapato halisi ya serikali.

Katika hatua nyingine, Almas amesema endapo NRA itashika dola, wananchi watapata huduma ya maji bure kwa kutumia teknolojia kutoka nje ya nchi na njia mbadala kama nguvu ya upepo kupeleka maji kwa wananchi.

Aidha, Almas amesema NRA pia itahakikisha wanasiasa wanapungua kwenye maisha ya watu kwa kupunguza baadhi ya Wizara na kuziweka sehemu moja itakayoendeshwa na wasomi wenye taaluma husika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button