David Mulokozi afurahia uwekezaji Manyara

MANYARA: Wawekezaji mkoani Manyara wamemkaribisha kwa kishindo mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk Samia Suluhu Hassan mkoani humu katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kampeni mkoani humo.

Akizungumza baada ya kutua kwa helikopta inayohamasisha wananchi kumchagua Dk Samia, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands LTD, David Mulokozi ameeleza kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia mazingira ya uwekezaji yameboreshwa zaidi nchini hali iliyopelekea wawekezaji wa ndani na nje kuongezeka.

Amesema mazingira mazuri ya uwekezaji yamevutia watu wengi kuwekeza na kutoa fursa za ajira na kuinua uchumi wa nchi husika.
Dk Samia Suluhu Hassan leo yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kampeni katika Wilaya ya Babati katika viwanja vya stendi ya zamani.



