Maeneo 7 historia ya ukombozi Afrika yawa urithi

SERIKALI ya Tanzania imeyatangaza maeneo ya historia ya ukombozi wa Afrika na Hifadhi ya Malikale kuwa urithi wa taifa ili yatambuliwe, yahifadhiwe na kulindwa kisheria.

Maeneo hayo yametangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na 582 Toleo la Septemba 26, 2025 ambalo lilisainiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana Agosti 26, 2025.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa katika Tangazo la Serikali ni kambi ya wapigania uhuru wa Chama cha African National Congress (ANC) iliyopo Mazimbu, Morogoro, Kambi ya wapigania Uhuru wa chama cha Frelimo iliyopo katika Shule ya Sekondari Samora Machel.

Mengine ni kambi ya wapigania uhuru ya Kihesa Mgagao, Makazi ya Mtemi Fundikira na Mtemi Isike.

Serikali imeendelea kuyatangaza maeneo ya kihistoria na Hifadhi ya Malikale kupitia notisi ya Gazeti la Serikali ya kutangaza maeneo ya hifadhi ya malikale kupitia Kifungu cha 3 (2) cha Sheria ya Malikale.

Kifungu kinatoa mamlaka kwa wizara yenye dhamana ya Malikale kuanzisha na kutangaza maeneo ya hifadhi ya Malikale nchini ili kuwa urithi wa taifa na baadaye kutangazwa kuwa urithi wa dunia.

Hatua ya kutangazwa kwa maeneo hayo inalenga kuyatambua, kuyahifadhi na kuyalinda kupitia sheria ya malikale na kutangazwa kuwa maeneo ya kichocheo cha vivutio vya utalii wa kihistoria nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button