Tanesco, Saccos yanufaisha wanachama mikopo bil 27.2/-

MOROGORO: CHAMA cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO SACCOS) kimetoa  mikopo ya zaidi ya Sh bilioni 27.2 kwa wanachama wake kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2025.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Saccos ,Omari Shaaban amesema hayo kupitia taarifa yake kwa wanachama wakati wa mkutano mkuu wa 57,wa mwaka uliofanyika mjini Morogoro.

Shaaban amesema mikopo hiyo imetolewa kwa wanachama 4,031 kuanzia Januari hadi Agosti  mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya uanzishwaji wake katika kuwasaidia kiuchumi.

“Katika kipindi cha kushia Agosti 31, 2025 chama kimetoa mikopo kwa wanachama yenye thamani ya Sh 27, 257,207,164  na  mikopo hiyo iliyotolewa kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyowekwa na chama kupitia sera ya mikopo,” amesema Shaaban .

Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Saccos amesema licha ya kupitia sera za mikopo pia ikiwemo kufanya tathmini ya uwezo wa mkopaji, kuhakikisha kuwepo kwa wadhamini wa kuaminika, na kuzingatia uwezo wa marejesho ya kila mwanachama.

Kwa upande wa suala la mtaji amesema kuwa mtaji wa chama umeongezeka kutoka Sh bilioni  4.9 mwaka 2023 hadi kufikia Sh bilioni 7. 1 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 75.

Kuhusu hisa za wanachama kwa mwaka ulioishia Disemba, 31, 2024 amesema kuwa ziliongezeka kwa asilimia tano na kufikia kiasi cha sh 11,184,586,538 ukilinganisha na mwaka 2023 ambapo zilikuwa na thamani ya sh 10,626,604,028.

Mwenyekiti huo wa Bodi amesema akiba za wanachama  zimeongezeka kutoka sh 44, 740,370,548  kufikia Desemba 31, 2023  hadi kufikia sh 46, 969,178,033  Desemba 31, mwaka 2024 na kufanya ongezeko la asilimia tano  na kikifanya Chama kimetoa faida juu ya akiba kiasi cha sh 907,161,712.

Mbali na hayo amesema licha kutoa mikopo kwa wanachama wake chama hicho kimekuwa kikitekeleza msingi was aba wa vyama vya ushirika unahimiza vyama kujali jamii inayowazunguka ili kuweka mahusiano na kuchangia maendeleo ya jamii.

Shaaban amesema kwa kutekeleza suala hilo kwa mwaka 2025 Chama kimechapisha shuka kwa ajili ya kusambazwa katika hospitali  za mikoa na Rufaa nchini.

Mwenyekiti wa Bodi wa Chama hicho amesemakuwa jumla ya sh milioni 23 zimetolewa na kuchapa shuka 1,300 zilizosambazwa katika hospitali za jiji la Dodoma na mpango huo utakuwa ni endelevu kwenye mikoa mingine nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, wakati wa ufunguzi mkutano mkuu huo, Naibu  Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji wa Shirika hilo, Mhandisi Antony Mbushi amesema Tanesco inajivunia uwepo wa Saccos hiyo.

Mhandisi Mbushi ameutaka uongozi kuendelea kutoa misaada kwenye maeneo mengine ili kuhakikisha wanafikia lengo na kutoishia utoaji wa shuka pekee kwenye hospitali bali na kwa watu wenye mahitaji wengine.

Naye mjumbe wa mkutano huo kutoka Kahama, Shinyanga, Wilson Kingu amesema saccos yao  ni mkombozi kwao kiuchumi kwani yeye binafsi anauwezo wa kukopa fedha kiasi kikubwa na kurejesha.

Kwa upande wake mwakilishi mkutano huo kutoka mkoa wa Morogoro, Neema Francis ametoa wito kwa Wafanyakazi wenzake kujiunga kwenye chama kwani kinasaidia katika maisha binafsi na kupiga hatua kwa haraka kupitia Tanesco Saccos.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button