Kariakoo yatangaza msamaha wa kodi miezi miwili

SHIRIKA la Masoko Kariakoo mkoani Dar es Salaam limetangaza msamaha wa kodi wa miezi miwili kwa wafanyabiashara waliounguliwa na maduka.
Meneja Mkuu wa shirika hilo, Ashiraf Abdulkarim ametangaza msamaha huo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka 2025 Dar es Salaam.
“Wafanyabiashara waliounguliwa na maduka yao wanaruhusiwa kuanza kuyajenga upya na hatutawalipisha kodi kwa miezi miwili ijayo. Hii ni kwa lengo la kuwasaidia kurudi katika shughuli zao bila vikwazo,” amesema Abdulkarim.
Amesema wamezindua wiki hiyo ili kutoa huduma za karibu kwa wafanyabiashara na kusikiliza changamoto zao.
“Niwahakikishie hatutamwacha mfan- yabiashara yeyote aliyekuwa na eneo lake hapa Kariakoo. Wiki hii ni ya kuwahudumia kwa ukaribu zaidi na kuhakikisha wanarejea katika biashara zao kwa usalama,” amesema Abdulkarim.
Amesema zaidi ya maeneo 400 ya kuegesha magari yameandaliwa kusaidia usafiri na shu- ghuli za biashara ndani ya soko.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam, Omary Yenga amesema soko jipya la Kariakoo ni mwanzo wa mapinduzi ya kibiashara ndani na nje ya Tanzania.
“Biashara haiwezi kukamilika bila soko. Tunashukuru kwa kuwa na soko kubwa lenye thamani, miundombinu bora na ulinzi wa kutosha. Hili litachochea ukuaji wa uchumi wa taifa,” amesema Yenga.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Karia- koo, Severine Mushi amesema ofisi za uongozi wa wafanyabiashara zitakuwa ndani ya soko hilo.
“Tunatarajia kukuza uchumi wa nchi kupitia soko hili. Kwa changamoto tulizopitia, tungependa hata kuanza kulipia kodi Januari ili tuweze kujipanga vyema,” amesema Mushi.
Mwenyekiti wa Wamachinga, Steven Lusinde ameahidi ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha wateja wanapata huduma bora sokoni.
Meneja wa Soko la Kisutu, Happy Njovu ametoa shukrani kwa uongozi wa Kariakoo kwa jitihada za kuboresha mazingira ya biashara.

Get 560000000 jokes videos with zero subscriber and zero View… But getting $34,000 per hour………. https://youtube.com/shorts/Xo0zswJ3qZQ?si=6c_7GFS8iVXdUTmT