Mikakati 5 ya serikali kukabili afya ya akili

DAR ES SALAAM: WIZARA ya Afya imesema kuwa imeandaa mikakati mitano ya itakayosaidia kuhakikisha inapambana na changamoto ya afya ya akili inayosababisha na majanga mbalimbali kama vile migogoro, maporomoko na magonjwa ya mlipuko.

Akitoa taarifa katika kuadhimisha Siku ya Afya ya Akili Duniani leo Oktoba 10, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Maghembe amesema serikali imeanzisha madawati ya msaada wa kisaikolojia ,kuwajengea uwezo wahudumu wa afya wa ngazi ya msingi ,kushirikiana na viongozi wa dini ,vyombo vya habari  na mashirika ya kijamii katika kutoa elimu kwa umma  na kupambana na unyanyapaa dhidi ya wenye changamoto za afya ya akili

“Tanzania inaungana na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na nchi wanachama katika kuadhimisha siku ya afya ya akili duniani .Kaulimbiu ya mwaka huu ni “upatikanaji wa huduma za afya ya akili wakati wa majanga na dharura “ikiwa na ujumbe mahususi wa kuhimiza huduma za afya ya akili na msaada wa saikolojia na kijamii kutolewa kwa watu wote hususan walioathirika na majanga kama mafuriko ,maporomoko ya ardhi ,milipuko ya magonjwa,migogoro na ajali za barabarani,”ameeleza.

Dk Maghembe amesema kwa mujibu wa WHO Mwaka 2025 watu takribani milioni 1 duniani wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na migogoro ,mabadiliko ya tabianchi  na majanga ya asili .

Amebainisha kuwa kati yao zaidi ya milioni 300 wanahitaji huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia jambo linaloonesha ongezeko kubwa la mahitaji haya muhimu.

Aidha amefafanua kuwa hapa nchini athari za kisaikolojia zinaonekana wazi wakati wa majanga mbalimbali kama mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyotokea Hanang Mkoa wa Manyara 2023 ambapo watu zaidi ya 5,600 waliathirika moja kwa moja .

“Katika tukio hilo serikali kwa kushirikiana na wadau iliwafikia watu 3,380 kwa msaada wa kisaikolojia na kijamii,huduma hizi zimetolewa pia katika majanga mengine kama mlipuko wa COVID -19 ,Mpox,Mrburg na maporomoko ya majengo,”amesema.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kutambua kuwa huduma za afya ya akili ni haki ya msingi ya kila mtu hivyo wawasaidie wanaokumbwa na changamoto hizo kwa kuwasikiliza bila kuwahukumu ,kuwahamasisha kutafuta msaada na kushirikia katika kujifunza kuhusu afya ya akili.

“Tujenge jamii yenye huruma ,matumaini ,mshikamano na upendo,”amesisitiza .

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button