Samia atoa somo wanaodharau wanawake

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ametaka watu wasibeze kuongozwa na rais mwanamke, kwani mwanamke na mwanaume wote wanafikiri sawa.
Samia aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Samia kufika Serengeti tangu mwaka 2010.
Alisema hivyo kwa sababu amesikia maneno kwamba CCM wameleta mgombea mwanamke, huku mila na desturi hazitaki mgombea mwanamke.
“Pamoja na mila na desturi zenu, suala la umoja na mshikamano wa Watanzania ni suala muhimu sana… lakini vilevile Mungu alivyotuumba hakuumba mwenye kichwa fulani alichozaliwa nacho kwamba ana akili kuliko mwenzake… hatukuambiwa mwanamke ana akili zaidi kuliko mwanaume au mwanaume ana akili zaidi kuliko mwanamke,” alisema.

Alisema Mungu alitofautisha jinsi hizo mbili kwenye kazi alizowapa, ambazo mwanamke ni kubeba ujauzito na kuzaa kwa uchungu na akamuumba na maumbile hayo.
“Wanaume mkaambiwa nyinyi ni wasimamizi wa wanawake na mtafanya kazi ya kutunza familia zenu lakini jinsi tunavyokwenda, wanawake wanafanya kazi na kutunza familia zao,” alisema.
Aliongeza: “Kwenye maendeleo ndugu zangu hakuna mwanamke, hakuna mwanaume. Mimi ninayesema hapa ni rais, ndani ya miaka minne nimefanya makubwa sana, ingekuwa mwanamke hawezi nisingeweza kuyafanya yote niliyofanya… tena mwanamke ni mwaminifu zaidi na mtendaji zaidi kwa sababu ya uoga kuliko mwanaume”.
Alisema Tanzania itaendeshwa na kuendelezwa mambo yake na wanaume na wanawake wote kwa umoja wao, cha muhimu ni wote Watanzania, wote wa taifa moja.
“Tushikamane tuijenge nchi yetu kama waasisi wetu walivyotuambia, yale ya huyu mwanamke huyu mwanaume hayapo… ulimwengu unajengwa na wanawake na wanaume. Kuna wanasayansi wanawake na wanaume, kuna madaktari wanawake na wanaume na unapokwenda hospitali husemi huyo daktari mwanamke asinitibu, unatibiwa na mwanamke na mwanaume,” alisema.
“Unapolindwa na askari wetu, unalindwa na wanawake na wanaume au tumesema askari wetu wanawake hawafai kulinda? Wanapangwa malindo na Tanzania yetu ipo salama… hata mimi nilipoingia kuna waliobeza kwamba sitoweza, leo tunazungumza mengine,” alisema.
Akiomba kura katika wilaya hiyo, Samia alisema Serengeti ni mji wa mkakati wa utalii kutokana na kuzungukwa na hifadhi na mkakati wa kuitunza hifadhi hiyo, hali inayovutia watalii na kufanya hifadhi hiyo kupata tuzo za kimataifa mara kwa mara.
“Sasa katika miaka mitano inayokuja, mkitupa ridhaa na mkituchagua, lengo letu katika utalii ni kuendelea kutangaza vivutio vyetu na kukuza utalii kufikia watalii milioni nane kwa mwaka ifikapo mwaka 2030,” alisema.
“Hivyo basi Hifadhi ya Taifa ya Serengeti itakuwa sehemu muhimu ya kufikisha watalii hao milioni nane,” alisema na kuahidi kujenga kiwanja cha ndege kama ilivyoelekeza ilani ya uchaguzi ya chama chake.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website
Open This…. https://Www.Work99.site