Nyerere: Aliyekichukia fedha na anasa

TUNARUDI kwa Sheikh Mohamed Said, mtunzi nguli wa vitabu, mwandishi mkongwe, mwanahistoria na mtaalamu wa sayansi ya siasa anayeendelea kutoa simulizi adimu kuhusu maisha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika moja ya mazungumzo yake ya kihistoria, Sheikh Mohamed Said anaeleza namna Mzee Dossa Aziz, mmoja wa wapigania uhuru, alivyomuelezea Mwalimu Nyerere kuwa mtu asiyekuwa na tamaa ya fedha wala maisha ya anasa.

Kwa mujibu wa simulizi hiyo, Mzee Dossa Aziz, akiwa nyumbani kwake Ruvu, mkoani Pwani, alimsimulia, Sheikh Mohamed Said, kwamba Nyerere alikuwa mtu muaminifu kupindukia  kiasi kwamba ukiweka kitita cha fedha kwenye bahasha na kumkabidhi, kesho yake ungezikuta zikiwa vile vile.

Mzee Dossa anakumbuka walivyokuwa wakikutana kila asubuhi katika mitaa ya Mkwepu na Makunganya, jijini Dar es Salaam, kujadili masuala ya chama cha TAA na baadaye TANU, wakati harakati za kupigania uhuru zikiwa zimepamba moto katika miaka ya 1950’s. SOMA: Dk. Salim asisitiza amani, kumuenzi Mwalimu

Katika simulizi hiyo, Mzee Dossa Aziz anamtofautisha Nyerere na viongozi wengine wa Kiafrika waliotawaliwa na tamaa ya madaraka na anasa, akimtaja kwa mfano Mobutu Sese Seko wa Zaire, aliyekuwa akijulikana kwa utajiri wa kupindukia.

Aidha, Sheikh Mohamed Said amegusia pia namna Mwalimu Nyerere alivyoshiriki binafsi katika kurudisha mwili wa aliyekuwa Waziri wake, Abdulrahman Mohamed Babu, aliyefariki dunia nje ya nchi. Licha ya wawili hao kuwahi kutofautiana kimtazamo kuhusu masuala ya kiitikadi na kiuchumi.

Simulizi hii inasisitiza taswira ya Mwalimu Nyerere kama kiongozi mnyenyekevu, mzalendo na mwenye misingi ya maadili isiyotetereka, ambaye hata wapinzani wake wa kisiasa walimtambua kwa uadilifu na utu wake.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Make money while staying at home and working online. I just received $23,783 for my work last month, and I was doing this part-time. This year, I plan to earn even more, and I believe you can also make extra cash from this job. To join right now, follow the details on this website.

    Open This… http://Www.Work99.Site

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button