Mradi wa bil 96/- wazinduliwa kukabili magonjwa ya mlipuko

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amezindua mradi wa dunia wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko nchini na kuzitaka wizara zote, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na taasisi kutekeleza shughuli za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura za kiafya.
Dk Biteko ametoa agizo hilo jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 38.7 (takribani Sh bilioni 96), unalenga kuboresha huduma za afya kwa Watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi.
Amesisitiza kuwa wizara, taasisi na washirika wa maendeleo wanatakiwa kusimamia utekelezaji katika uwekezaji huo na kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.
“Wizara zote, tawala za mikoa na taasisi, tekelezeni shughuli zote za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa haya ya mlipuko na dharura nyingine za afya kulingana na maeneo yenu na hakikisha kwamba
hakuna hata Shilingi moja inayopotea au kuchepushwa kando ya malengo yaliyokusudiwa,” amesema.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amesema mradi huo unatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia sehemu ya afya, pamoja na wadau wa maendeleo, likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) na Pandemic Fund.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya ambaye ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Magembe amesema mradi huo utaboresha mwitikio wa mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa kama Ebola, Virusi vya Homa ya Nyani, Marburg, Zika na magonjwa mengine yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Dk Magembe amefafanua kuwa utekelezaji madhubuti utawezesha upatikanaji wa taarifa za haraka kuhusu uwepo au uvumi kuhusu magonjwa ya mlipuko na hivyo kuzifanyia kazi taarifa hizo.
Amesema upatikanaji wa fedha hizo utawezesha pia uboreshaji ya maabara ya taifa na kikanda, ikiwa ni njia ya kupata taarifa za haraka kwa usahihi kutoka kwa wananchi.
Akizungumzia utekelezaji wa mpango huo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Salim Nassor Slim aliwashukuru viongozi wa kitaifa kwa hatua za kuboresha afya za wananchi kuwa na afya bora.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com