TOSCI yatoa elimu kutambua mbegu bandia

TAASISI ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi, wakulima na wadau wa sekta ya kilimo kuhusu utambuzi wa mbegu bora, taratibu za usajili wa wazalishaji wa mbegu, pamoja na namna ya kuepuka mbegu bandia sokoni.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya TOSCI kushiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Chakula Duniani yanayofanyika jijini Tanga kuanzia Oktoba 10 hadi 16, ikiwa na lengo la kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu bora kwa ajili ya kilimo chenye tija.

Mkurugenzi wa Majaribio na tathmini wa TOSCI,Matengea Swai amesema wanafanya kazi ya usajili  wafanyabiashara wote wa mbegu, aina zote za mbegu kupitia majaribio ya utambuzi wa aina mpya ya mbegu, majaribio ya umahiri wa mbegu ili kuweza kusajia aina mpya za mbegu. “Baada ya aina mpya tunaangalia tunaitambuaje na faida mbegu kwa mkulima wetu baada ya kupitiwa na kamati mbalimbali tunamshauri waziri wa kilimo aipitishe na kutangazwa kutumika kwa wakulima.

Ameongeza “Baada ya mbegu hiyo tunasajili kwenye daftari ya aina mpya ya mbegu ambalo linapatikana website ,mbegu inaongezeka ili iweze kumfikia mkulima inaingea kwenye sehemu ya udhibiti wa mbegu ,”amesisitiza Swai. SOMA: TCB yaondoa hofu upatikanaji mbegu bora za pamba

Amesema katika  sehemu hiyo  wanasajili mashamba ya mbegu na kwenda kukagua na baadae wanaenda kuchukua sampuli  kufanya majaribio ya mbegu maabara ambapo wanaangalia uotaji wa mbegu ,usafi na afya ikiwa safi wamekamilisha .

Aidha, wananchi waliotembelea banda la TOSCI wamepata fursa ya kuuliza maswali na kujifunza kwa vitendo kuhusu hatua mbalimbali za uthibitishaji wa mbegu, jambo linalolenga kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa uzalishaji wa mbegu bora unaochangia usalama wa chakula na maendeleo ya kilimo nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button