RC Chalamila akagua miundombinu Tanesco

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea kituo kikuu cha kuzalisha umeme cha Shirika la Umeme ( Tanesco) kilichopo Ubungo jijini Dar es salaam pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Mabibo na Mbagala.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amesema mkoa huo pekee Serikali imewekeza takriban Sh trilioni 1.3 kwenye sekta ya umeme.

Amesema suala la kukatika umeme kwa sasa sio kwa sababu ya upungufu wa umeme bali ni maboresho ya miundombinu hususani baada ya Rais Dk Samia kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere.
Aidha, RC Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kushirikiana na Serikali kulinda miundombinu ya shirika la umeme, isiharibiwe ili kuendelea kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwani shughuli zote za kiuchumi na uwekezaji zinahitaji uimara kwenye sekta ya umeme.

Vilevile RC Chalamila ameendelea kuwakumbusha wakazi wa mkoa huo na watanzania waliojitokeza kwenye ziara hiyo kuwa Octoba 29 mwaka huu ni siku ya uchaguzi hivyo kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze kupiga kura kwa kwa amani huku akiwatahadharisha wote wenye nia ya kuleta vurugu kuwa Serikali haitowavumilia.

Naye, Naibu Mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme nchini TANESCO kwa upande wa usambazaji umeme Mhandisi Atanasius Nangali ameeleza namna serikali mkoani humo ilivyoongeza uwekezaji kwenye uzalishaji umeme huku Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando aliposhiriki ziara hiyo amesema uwekezaji wa umeme unaofanyika umekuwa na manufaa makubwa kwenye kuboresha maisha na kuongeza ajira kwa vijana




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com