Watanzania kupatiwa huduma za afya kwa simu

DAR ES SALAAM: Katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi Kampuni ya Bima ya Afya ya Jubilee Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Afya ya Medikea wameanzisha programu maalumu inayowezesha Watanzania kupata huduma za afya kwa njia ya simu popote walipo.
Programu hiyo iliyozinduliwa Dar es Salaam Oktoba 16, 2025, inalenga kuimarisha afya za Watanzania kwa kuwapatia huduma za kiafya kupitia teknolojia ya mawasiliano, hususani simu za mkononi pia ikijikita katika kudhibiti usugu.
Aidha, itajikita katika kutoa huduma za afya kwa njia ya simu ikiwemo utambuzi na matibabu bila kuonana na daktari uso kwa uso.
Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye ni mtaalamu wa afya na mazoezi wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasioambukiza Tanzania (TANCDA), Dk Waziri Ndonde alisema magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari na saratani yamesalia kuwa miongoni mwa visababishi vikuu vya vifo vya mapema nchini vinavyohitaji kufanyiwa kazi kuvizui na kugunduliwa mapema kwa ushirikiano wa sekta zote.
Alisema programu hiyo inasimama kama mshirika mkubwa katika kutekeleza dhamira hiyo.
“Inaimarisha mikakati yetu ya huduma ya afya ya msingi na afya ya kiidijitali, kukuza huduma jumuishi na zinazomzingatia kila mmoja kwa Watanzania wote.
Alisema ni wakati wa wadau wote kushirikiana katika kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na ufahamu na anishi na kula kwa kufuata kanuni za afya.
Alisema katika Medikea Afya App Limited, maono yao ni kufanya huduma ya afya ipatikane na iendelee hivyo ushirikiano huo na Jubilee Health unaweka msingi wa siku zijazo.
Naye Mkuu wa Ustawi na Uhusiano wa Biashara wa Medikea, Dk Lilian Valerian alisema programu hiyo ni mwanzo wa mapinduzi ya huduma za afya na kwamba kwa sasa watu wahama kutoka mfumo ambao unasubiri mtu augue kwenda ule ambao unatembe na watu katika kila hatua ya safari ya kiafya.
Alisema jukwaa hilo la matibabu ya kidijitali litasaidia wateja wanaohudumiwa na bima ya afya ya Jubilee kupata huduma za afya ikiwemo ushauri wa madaktari bingwa popote walipo nchini kupitia simu zao za mkononi.
Mmoja wa wanufaika wa programu hiyo Jane Mwangoma alisema alipata tatizo la shinikizo la damu akiwa kazini, hali iliyomsumbua hadi kuamua kuacha kazi na baadaye kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikutana na programu hiyo.
“Ilikuwa kama muujiza, maana nilipofika pale wakaniambia tungependa tukusaidie zaidi. Ndipo wakagundua kumbe nina kisukari cha aina ya pili, kitu ambacho sikuwahi kujua awali,” alisema.
Alisema kupitia programu hiyo, alipewa vifaa vya kujipima kiwango cha sukari nyumbani na kupewa ushauri wa lishe na mazoezi, sasa hali yake imeimarika na anaweza kujihudumia vizuri.
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com