Serukamba: Nitatekeleza ahadi zangu zote

KIGOMA: MGOMBEA ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Peter Serukamba amesema kuwa atatekeleza ahadi zake zote ndani ya miaka mitano za kuwaletea wananchi maendeleo katika jimbo hilo alizotoa wakati wa mikutano yake ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Serukamba alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mkutano uliofanyika kwenye soko la Mwandiga Halmashauri ya Wilaya Kigoma na kuthibitisha kuwa anatoa ahadi ambazo zinaweza kutekelezwa na siyo kwa ajili ya kuongea uongo ili achaguliwe katika uchaguzi huo.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) Peter Serukamba akizungumza na wapiga kura wa jimbo hilo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika soko la Mwandiga Halmashauri ya Wilaya Kigoma.

Katika mkutano huo, Serukamba alizitaja ahadi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari mpya saba ambapo moja itajengwa kwenye mji mdogo wa Mwandiga, madarasa mapya ya shule za msingi, ukarabati wa shule kongwe, ujenzi wa matundu 467 katika shule za sekondari 150 na ujenzi wa nyumba za walimu 15.

Sambamba na hayo, Serukamba alisema katika sekta ya afya ataweka kipaumbele kumalizia ujenzi wa hospitali ya wilaya iweze kutoa huduma kikamilifu, ujenzi wa vituo vipya vya afya saba katika jimbo hilo, kumalizia ujenzi wa zahanati kila kijiji sambamba na uwepo wa huduma za baba,mama na mtoto katika zahanati hizo.

Aidha katika suala la Miundo mbinu alisema kuwa atahakikisha zinajengwa barabara za kiwango cha lami katika mji mdogo wa Mwandiga, barabara ya kiwango cha Lami kutoka Mwandiga hadi Kagunga, barabara ya lami Simbo hadi Ilagala, barabara ya kiwango cha Lami kutoka Mahembe hadi Bitale sambamba na kukamilisha upelekaji umeme katika vijiji vyote vya jimbo hilo.

Mgombea huyo alisema kuwa ameshakuwa mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 15, amekuwa Mkuu wa mkoa katika mikoa tofauti lakini pia kablaa hapo alikuwa mtendaji Mwandamizi wa serikali hivyo anajua mahali pa kuingilia na kutokea ili ahadi hizo ziweze kutekelezwa.

Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata ya Mwandiga, Deusdedith Alphonce akizungumza katika mkutano huo wa kampeni alisema kuwa CCM ndiyo chama pekee chenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo Watanzania hivyo ametaka wapiga kura kuchagua wagombea wa chama hicho badala ya kuchagua madalali.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. I am making a good s­al­ary from home $4580-$5240/week , which is amazing und­er a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now its my duty to pay it forward and share it with Everyone,Here is I started_______ https://cashprofit7.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button