Safari za SGR zarejea

SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) linawajulisha umma kuwa shughuli za huduma za treni za SGR zimerejea tena. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Reli Tanzania Fredy Mwanjala imesema kuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC ) linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza wa usafiri huo.
Taarifa hii inakuja baada ya kutokea ajali katika eneo la Pugu jijini Dar- es-salaam kutokana na hitilafu ya uendeshaji iliyotokea. SOMA: SGR Uvinza-Musongati, funguo muhimu milango mipya ya uchumi