Nchimbi: Asiyempigia kura Samia hana nia njema

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema yeyote atakayekataa kumpigia kura mgombea wake wa urais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hana nia njema na maendeleo ya taifa. Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi amesema Samia amefanya kazi kubwa na ni ushahidi kwamba ana uwezo wa kusukuma mbele maendeleo ya Watanzania.
Dk Nchimbi alisema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya juzi. “Ni mtu asiyependa maendeleo peke yake anayeweza kumnyima kura Rais Samia. Kama mtu anapenda maendeleo kwelikweli, lazima atampigia kura Samia na Chama Cha Mapinduzi,” alisema.
Dk Nchimbi alisema wananchi wa Makongolosi na Chunya kwa ujumla wanajulikana kwa kupenda maendeleo hivyo hatarajii kura ya kupinga. Alisema ushirikiano wa Samia na viongozi wa ngazi zote Chunya umewezesha mafanikio, hususani kwenye kilimo na madini katika Jimbo la Lupa.

Dk Nchimbi alisema katika sekta ya kilimo, serikali imewekeza kwenye vipimo vya kisasa vya udongo na kuongeza uzalishaji wa chakula na akasema Mkoa wa Mbeya umeongeza mavuno maradufu. Alisema katika sekta ya madini, Samia ameweka mkazo kwa wachimbaji wadogowadogo na kwa Chunya kuna zaidi ya leseni 1,225 halali. Pia, Dk Nchimbi alisema Hospitali ya Wilaya ya Chunya imeboreshwa na sasa inatoa huduma bora kwa wananchi.
Alitaja miradi mipya inayotarajiwa kutekelezwa, ukiwemo wa kubadilisha hospitali ya wilaya kuwa ya kiwango cha juu zaidi na ununuzi wa mitambo ya kuzalisha hewa tiba. Pia, Dk Nchimbi alisema serikali itajenga zahanati mpya tano, vituo vipya vya afya vitano pamoja na nyumba za watumishi wa kada ya afya saba.

Katika upande wa elimu ya afya, alisema kitajengwa chuo cha wauguzi katika eneo hilo ili kuongeza nguvukazi ya afya. Kwa upande wa kilimo, alisema serikali imepanga kujenga skimu mpya za umwagiliaji pamoja na maghala sita ya kisasa ya kuhifadhia nafaka.
Dk Nchimbi alisema serikali itaendeleza ajenda ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata leseni kwa urahisi sanjari na kuwapa elimu ya ujasiriamali. SOMA: Mwinyi afunga kampeni Pemba, aeleza vipaumbele 10 vya maendeleo




Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/