Mradi wa bil 94/- kukabili gesijoto, kulinda viumbe
SERIKALI imezindua mradi wa kukabili mabadiliko ya tabianchi na kulinda bayoanuai wenye lengo la kupunguza gesijoto na kulinda mfumo wa viumbe hai.
Mradi huo wa thamani ya Sh bilioni 94 unatekelezwa kwa ushirikiano katiya Serikali ya Tanzania, Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF).
Akizungumza Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha kamati ya usimamizi wa mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi amesema mradi huo ni matokeo ya kukubalika kwa sera za Tanzania katika kukabiliana na changamoto za mazingira kimataifa.
“Mradi huu ni muhimu na unaoashiria kwamba, kwanza sera zetu za nchi kwenye kukabiliana na changamoto mbalimbali za mazingira zinakubalika kimataifa, kwa sababu hii miradi ipo michache duniani na ni miradi ya ushin- dani kuweza kupata fedha za utekelezaji,” amesema Dk Abbas.
Amesema awamu ya kwanza ya mradi itatekelez- wa katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, ikihusisha hifadhi za Amani, Magamba, Nilo na Chome ambayo ni maeneo yenye utajiri mkubwa wa misitu na vyanzo vya maji.
Dk Abbas amesema zaidi ya asilimia 40 ya ardhi ya Tanzania imehifadhiwa kwa ajili ya misitu na mapori ya akiba, jambo linaloifanya Tanzania kuwa kati ya nchi zinazoongoza katika uhifadhi duniani.
Kutokana na juhudi za uhifadhi, alisema idadi ya watalii waliotembelea misitu imeongezeka kutoka 59,000 mwaka 2020/2021 hadi 346,000 mwaka 2024/2025 na mapato yamepanda kutoka Sh mil- ioni 154 hadi Sh bilioni 2.8.
Akizungumzia mradi huo, Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema mradi huo ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2025–
2030) utachochea matumizi ya nishati safi ya kupikia, usafiri wa umeme na uwekezaji wa kijani katika hifadhi nchini.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Shigeki Komatsubara amesema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa miradi ya Net-Zero na Nature-Positive.
“Ushirikiano wetu na serikali unalenga kulinda misitu, kuimarisha nishati safi na kuboresha maisha ya wananchi,” alisema Komatsubara.
Katika utekelezaji wa mradi GEF imetoa Dola za Marekani milioni 4.7, UNDP imechangia Dola za Marekani 200,000 na serikali na wadau wengine wakichangia zaidi ya Dola za Marekani milioni 29 kupitia miradi ya uhifadhi na nishati safi.




Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/