Bakwata yawataka Waislamu kupiga kura

BARAZA Kuu Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Dodoma limewataka mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha wanahamasisha waumini wao misikitini kwenda kutumia haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi watakaofaa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Wilaya ya Dodoma, Bashiru Omary alisema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi hao kwenye kikao cha utendaji kazi kilichoambatana na kuiombea nchi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo.
Omary aliwataka viongozi hao kuhakikisha elimu ya umuhimu wa kupiga kura inatolewa pamoja na kuhamasisha waumini kwenda kutumia haki yao hiyo ya msingi ili wakawachague viongozi wanaowapenda kwa ajili ya maendeleo. SOMA: Maaskofu, masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani
Aliwataka viongozi hao kwenye utekelezaji wao wa kazi watumie pia nafasi zao kuwaondolea hofu ya upotoshaji inayotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii feki kwa kuwahimiza wajitokeze siku hiyo ya kupiga kura.
“Bakwata tunaamini Oktoba 29 ni siku ya kupiga kura nchi nzima kwa ajili ya kuchagua rais, wabunge na madiwani, hivyo Baraza la Waislamu Wilaya ya Dodoma linawataka waumini wote wenye sifa ya kupiga kura wajitokeze bila hofu yoyote na msitishike,” alisema.
Mwenyekiti huyo pia aliwataka viongozi wa misikiti pamoja na waumini kuendelea kuuombea uchaguzi huo ili ufanyike kwa amani na utulivu na nchi iweze kuwapata viongozi wake watakaokubalika mbele za Mungu na watu wake.
Alisema pamoja na majukumu waliyonayo kama viongozi na waumini, Baraza la waislamu linawataka pia kuliombea jambo hilo kwa gharama zote kwa Mwenyezi Mungu ili kufanikisha kwa kuwapata wale watakaofaa kuongoza kwa vitendo kwa ajili ya nchi.
Kikao hicho pia kiliwataka vijana kutokubali kutumika kama madaraja ya kushabikia vyama vya siasa ambavyo havina sifa ya kuongoza zaidi ya kutaka kuchafua na kufanya vurugu zisizo na tija.




Freedom to work whenever I want — that’s what I love! I made $18,542 in a month doing this online. Check the details ———————⊃⫸ https://dailycash21.blogspot.com/