Wanafunzi 135,240 wapata mikopo

WANAFUNZI 135,240 waelimu ya juu na ya kati wamepata udhamini wa masomo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wa thamani ya Sh bilioni 426.5 kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha.

Dk Kiwia amesema fedha hizo ambazo ni awamu ya kwanza zitawanufaisha wanafunzi 135,240 wakiwemo wa shahada ya awali, stashahada na udhamini wa Samia kama mikopo na ruzuku.

SOMA: Serikali yaongeza bajeti mikopo elimu ya juu

“Shilingi bilioni 152 zitawanufaisha wanafunzi 40,952 waliopangiwa mikopo ya sha- hada ya awali na wanafunzi 5,342 waliopangiwa mikopo ya stashahada,” amesema.

Ameongeza: “Pia wanafunzi 615 ni wanufaika wa ruzuku ya udhamini wa masomo wa Samia waliopangiwa ruzuku yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.3. Wanafunzi hawa ni wapya wanaojiunga na taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kati nchini.”

Kwa mujibu wa Dk Kiwia, wanafunzi wengine 88,331 wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo katika vyuo vikuu nchini wamepangiwa mikopo ya Sh bilioni 271.2.

Hata hivyo, amesema Bodi ya Mikopo bado inaendelea kuchakata maombi ili kupanga mikopo na kutangaza awamu zinazofuata kwa siku za hivi karibuni, ili kuwawezesha wanafunzi waliopangiwa mikopo kuendelea na taratibu za kuwasili na kujisajili katika vyuo walikodahiliwa.

Amesema serikali imeshawapatia fedha kwa ajili ya kugharamia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya kati kwa kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanaopangiwa mikopo au ruzuku wanazikuta fedha vyuoni ambako wamedahiliwa, kujisajili na kisha watapokea fedha hizo ili wa some na kutimiza ndoto zao. Katika hatua nyingine,

Dk Kiwia alisema serikali imetenga Sh bilioni 916.7 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi 273,347.

Amesema kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 99,300 watakuwa wanufaika wa mwaka wa kwanza wa stashahada, sha- hada na udhamini wa masomo wa Samia huku wanafunzi wengine 174,047 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliopita.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button