JK awamwagia sifa Samia, Dk Mwinyi utekelezaji Ilani

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama cha vitendo. Kikwete amesema hayo katika Uwanja wa Jambiani, Mkoa wa Kusini Unguja wakati akihitimisha kampeni za CCM katika majimbo ya mkoa huo ya Tunguu, Chwaka, Uzini, Paje na Makunduchi.

Alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa uongozi wao na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika pande zote za Muungano. Kikwete alisema viongozi hao wameonesha uongozi wa wazi wa kisasa na wenye matokeo chanya kwa wananchi. “Wananchi wanampenda kiongozi anayesema ukweli na anayetekeleza. Dk Samia na Dk Mwinyi wameonesha uongozi wa vitendo,” alisema.

Amesema chini ya uongozi wa viongozi hao, huduma za jamii zimeimarika kwa kasi kubwa zikiwemo afya, elimu, maji na barabara. Alisema Zanzibar ya sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita. SOMA: Mwinyi ataja sekta 11 kipaumbele awamu ijayo

Ametaja mafanikio ni pamoja na kuongezeka upatikanaji wa maji safi kutoka shehia 54 hadi 62 na ongezeko la uzalishaji wa samaki kutoka tani 5,606 hadi tani 12,155. Pia, alitaja mafanikio katika elimu ambapo kiwango cha ufaulu wa kidato cha nne kimepanda hadi asilimia 98.5 huku shule, maabara na hospitali mpya zikijengwa maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba. “Hospitali za Kitogani, Mwera Pongwe na Makunduchi ni ushahidi wa kazi nzuri ya Serikali ya CCM,” alisema Kikwete.

Amesema CCM imeendelea kuwa chama cha kuaminika kwa Watanzania kutokana na utekelezaji wa ilani yake kwa vitendo na kwa ufanisi. “CCM si chama cha maneno, ni chama cha kutenda. Tumetekeleza Ilani yetu kwa zaidi ya asilimia 85 na miradi inayobaki inaendelea. Huu ndio uthibitisho kwamba ahadi za CCM ni deni, na tunalilipa kwa vitendo,” alisema Kikwete.

Amesema serikali ya CCM itaendelea kuimarisha uchumi, kuongeza ajira zaidi ya 350,000, kukuza sekta ya utalii na kuanzisha hifadhi ya mafuta Zanzibar kupitia Ilani ya 2025-2030 yenye kaulimbiu ‘Kazi na Utu, Tunasonga Mbele’.

Aliwahimiza wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara walinde amani na umoja uliopo, akisema CCM itaendelea kuendeleza misingi ya vyama vya Afro Shiraz Party (ASP) na Tanganyika African National Union (TANU) ya usawa, umoja na maendeleo kwa wote.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Just started this 3 weeks ago, and I already received my first check of $3,677 — pretty cool! It’s not a get-rich-quick thing, but if you can use a computer and internet and give some time each day, you can totally do this too. I was honestly surprised how real and simple it turned out to be.
    just check.…………> https://Www.Smartpay1.site

  2. Just started this 3 weeks ago, and I already received my first check of $3,677 — pretty cool! It’s not a get-rich-quick thing, but if you can use a computer and internet and give some time each day, you can totally do this too. I was honestly surprised how real and simple it turned out to be.
    just check.…………> https://Www.Smartpay1.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button