Tamati kampeni Uchaguzi Mkuu 2025

VYAMA vya siasa kesho vinamaliza kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Tanzania Bara. Kampeni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zilianza Agosti 28, mwaka huu kwa Tanzania Bara baada ya uteuzi uliofanywa Agosti 27 na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) mwaka huu.
Kampeni za uchaguzi kwa Zanzibar ngazi zote zilianza Agosti 28, mwaka huu na zinakwisha leo kupisha kura ya mapema kesho. Pia Agosti 27, mwaka kuu INEC iliteua wagombea ubunge kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wagombea udiwani kwa Tanzania Bara.
Kwa nafasi ya urais INEC iliteua wagombea 34 wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kutoka vyama 17 vya siasa vilivyochukua fomu za uteuzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. SOMA: Samia kuhitimisha kampeni kesho Mwanza
Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele alifanya uteuzi huo baada ya wanachama waliopendekezwa kutimiza masharti ya Ibara ya 39 (1), 41 na 47 (4) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 zikisomwa pamoja na Kifungu cha 34 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na 1 ya mwaka 2024.
Wagombea walioteuliwa ni Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Kiti cha Rais na Dk Emmanuel Nchimbi (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hassan Almas (kiti cha Rais) na Hamisi Hassan (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA).

Wengine ni Coster Kibonde (kiti cha Rais) na Aziza Haji Suleiman (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Makini (MAKINI), Gombo Samandito (kiti cha Rais) na Husna Mohamed Abdalla (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Mluya (kiti cha Rais) na Sadoun Khatib (kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha Democratic Party (DP) na Kunje Ngombale Mwiru (kiti cha Rais) na Shum Juma Abdalla (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP).
Wagombea wengine ni Saum Hussein Rashid (kiti cha Rais) na Juma Khamis Faki (kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Mwajuma Mirambo (kiti cha Rais) na Mashavu Alawi Haji (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) na Georges Bussungu (kiti cha Rais) na Ali Makame Issa (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Tanzania Democratic Alliance (ADA-Tadea).
Wengine ni Twalib Ibrahim Kadege (kiti cha Rais) na Abdalla Mohd Khamisi (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha United People’s Democratic Party (UPDP), na Doyo Hassan Doyo (Kiti cha Rais) na Chausiku Khatib Mohamed (Kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Majalio Paul Kyara (Kiti cha Rais) na Satia Mussa Bebwa (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Wilson Elias Mulumbe (Kiti cha Rais).
Shoka Khamis Juma wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wanachama wengine walioteuliwa ni Haji Ambar Khamis (kiti cha Rais) na Dk Eveline Munisi (kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCRMAGEUZI), David Mwaijojele (Kiti cha Rais) na asoud Ali Abdala (Kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha Kijamii (CCK).

Wengine Salum Mwalimu (Kiti cha Rais), Devotha Minja (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), na Yustas Rwamugira (kiti cha Rais) na Amana Suleiman Mzee (kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Doyo amesema kuwa kampeni zao zimeenda vizuri na mapokeo yamekuwa makubwa kwa wale waliowaendea kunadi sera zao. Amesema wamefanikiwa kuibua hoja nzuri na za maendeleo, hivyo wananchi wana mategemeo kwao.
Ameongeza kuwa wanatarajia kufunga kampeni zao leo wilayani Handeni katika Mkoa wa Tanga. Busungu amesema kampeni zao zimeenda vizuri na wamejitahidi kupita mikoa karibu yote nchini kutangaza sera zao.“Kampeni zimeenda vizuri, tumeanza mdogomdogo na kadiri tulivyokuwa tunakwenda ndiyo kadri wananchi walivyokuwa wanatuelewa na Mungu ametujalia tumetembelea mikoa mingi na watu wameonekana kuikubali na kuipenda ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka huu,” alisema.
Amesema changamoto kubwa ilikuwa ya kifedha ambapo karibu vyama vyote wamekumbana nayo na kueleza kuwa ilibidi kujibana ili waweze kupitia maeneo muhimu na kufanya mambo muhimu, jambo ambalo limewasaidia kufanikisha kampeni zao.
Amesema wanatarajia kumaliza kampeni zao leo Nyamagana mkoani Mwanza. Rwamugira alisema wanatarajia kutamatisha kampeni zao kesho mkoani Kilimanjaro. Kyara alisema chama hicho kitamaliza kampeni zake kesho Muheza mkoani Tanga. Mirambo alisema watamalizia kampeni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Kibonde alisema watamalizia kampeni kesho Mbezi mkoani Dar es Salaam. Saumu amesema watahitimisha kampeni kesho.




Just started this 3 weeks ago, and I already received my first check of $3,677 — pretty cool! It’s not a get-rich-quick thing, but if you can use a computer and internet and give some time each day, you can totally do this too. I was honestly surprised how real and simple it turned out to be.
just check.…………> https://Www.Smartpay1.site
Just started this 3 weeks ago, and I already received my first check of $3,677 — pretty cool! It’s not a get-rich-quick thing, but if you can use a computer and internet and give some time each day, you can totally do this too. I was honestly surprised how real and simple it turned out to be.
just check.…………> https://Www.Smartpay1.site