Kila la heri uhitimishaji kampeni, amani iendelee

LEO vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu nchini vinahitimisha rasmi kampeni zake, hatua muhimu inayoashiria ukomavu wa demokrasia ya Tanzania.

Kwa takribani siku 60, wagombea wa vyama tofauti wa nafasi za urais, ubunge na udiwani walishuhudiwa wakizunguka maeneo mbalimbali ya nchi wakinadi sera na mipango yao kwa wananchi.

Ni jambo la kupongezwa kuona kampeni hizi zilizozinduliwa Agosti 28, mwaka huu zikiwa zimefanyika kwa utulivu, busara na kuheshimiana tofauti na mazoea ya nyuma ya majukwaa ya kampeni kutawaliwa na misuguano ya kisiasa na lugha za kejeli.

SOMA: Tukemee wanaotaka kuleta vurugu uchaguzi mkuu

Tunazipongeza taasisi zote zilizosimamia mchakato huu, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), vyombo vya usalama, vyombo vya habari, viongozi wa dini, asasi za kiraia, na wananchi kwa ujumla.

Ushirikiano wao umesaidia kuhakikisha kwamba kipindi cha kampeni kinapita kwa amani, bila vurugu, na bila matukio makubwa ya uvunjifu wa sheria.

Tunaamini hata leo vyama vinapohitimisha kampeni zake, amani na utulivu utaendelea kutawala. Huu ni ushahidi kwamba Watanzania wameendelea kukomaa kisiasa na kutambua kuwa siasa ni chombo cha maendeleo na si uhasama.

Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, tunatambua kwamba hatua muhimu zaidi ipo mbele yetu kesho ambayo ni siku ya kupiga kura.

Tunawahimiza wananchi wote watumie haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu wakitambua kwamba uchaguzi ni fursa ya kuchagua viongozi watakaosimamia maslahi ya taifa na si uwanja wa kugombania au kuhasimiana.

Ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha anashiriki kwa utulivu, akiheshimu taratibu za uchaguzi na maelekezo ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.

Tunawakumbusha pia wanasiasa na wafuasi wao kwamba baada ya kura kupigwa, ni muhimu kusubiri matokeo kwa subira na heshima na INEC ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kutangaza matokeo rasmi.

Asiwepo yeyote wa kuvuruga amani kwa sababu yoyote ile. Amani ambayo Tanzania imejijengea kwa miaka mingi ndiyo msingi wa maendeleo, haitakiwi kuwekwa rehani kwa maslahi ya kisiasa.

Aidha, tunazihimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ziko kwenye maandalizi au mchakato wa uchaguzi ikiwemo Uganda ambayo inaendelea na kampeni, zichukue mfano wa Tanzania ambayo imeonesha kwamba inawezekana kufanya kampeni zenye ushindani wa hoja bila chuki wala vurugu.

Utulivu wa kisiasa ni nguzo muhimu katika kujenga uchumi wa kikanda na kuimarisha ushirikiano wa maendeleo ndani ya EAC.

Ni wajibu wa kila Mtanzania mwenye nia njema na nchi kuendelea kulinda heshima ya Tanzania ambayo inajulikana kuwa ni kisiwa cha amani si tu katika Afrika Mashariki bali barani.

Tuna imani thabiti kwamba hata uchaguzi wa kesho utakuwa wa amani, huru, na wa haki, na matokeo yake yataakisi matakwa ya wananchi wote.

Amani yetu ni urithi wa thamani ambao inatupasa kila mmoja kuuthamini na kuuimarisha kwa vitendo.

Atakayejitenga na dhamira hii, ahesabiwe ni adui wa maendeleo si kwa Tanzania pekee bali jumuiya nzima ya Afrika Mashariki.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button