Chalamila ataka wadau wafunze vijana umuhimu wa amani

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wadau na jamii kuendelea kutoa elimu kwa vijana hasa walio kwenye makundi ya waendesha pikipiki (bodaboda) na bajaji juu ya umuhimu wa kulinda na kudumisha amani jijini humo.
Kauli hiyo ya Chalamila imekuja siku chache baada ya kundi la vijana kufanya vurugu na kuharibu mali binafsi na za serikali katika mikoa mbalimbali nchini siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu.
Alisema Jiji la Dar es Salaam linahudumia nchi nyingi zisizo na bandari na lina shughuli nyingi za biashara, afya na uchumi, hivyo amani ni nguzo muhimu katika ustawi wake.
“Jamii iendelee kutoa elimu kwa vijana wetu hawa waelewe umuhimu wa amani na namna ya kuidumisha,” alisema.
Chalamila aliyasema hayo juzi alipokutana na wadau wa sekta ya nishati ya mafuta ya dizeli na petroli katika kikao maalumu kilichoratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Ubungo, Dar es Salaam.
Miongoni mwa waathirika wa vurugu za Oktoba 29 ni wamiliki wa vituo vya mafuta ambavyo vingi viliteketezwa na moto, taarifa zinasema takribani vituo 41 nchi nzima viliteketezwa kwa moto.
Katika kikao hiko, yalifanyika majadiliano ya kina kuhusu suala la ulinzi na usalama wa vituo vya mafuta kufuatia matukio hayo ya uhalifu.
Aidha, Chalamila alitoa pole kwa wafanyabiashara hao akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwa bega kwa bega nao kutokana na mchango mkubwa wanaotoa katika uchumi wa taifa na katika maisha ya wananchi mmoja mmoja.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com