Dk Nchimbi ahimiza amani Maziwa Makuu

SERIKALI ya Tanzania imesema amani na usalama ni muhimu kwa maendeleo ya ukanda wa maziwa makuu.

Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi amesema hayo wakati akichangia mjadala katika mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) jijini Kinshasa.

Alikuwa akichangia kaulimbiu ya mkutano huo isemayo: Kuimarisha Amani na Usalama kwa ajili ya Maendeleo Endelevu kwenye Eneo la Maziwa Makuu.

Dk Nchimbi alisema kaulimbiu hiyo inatambua ukweli wa msingi kwamba maendeleo ya kudumu hayawezi kupatikana bila amani na amani ya kudumu haiwezi kupatikana bila maendeleo jumuishi na endelevu.

Alisema eneo la Maziwa Makuu limebarikiwa na utajiri wa maliasili yakiwemo madini adimu na rasilimaliwatu, lakini linakabiliwa na migogoro ya kisiasa ya muda mrefu inayochochewa na uvunaji haramu wa maliasili.

Migogoro hiyo imesababisha majanga ya kibinadamu yakiwemo watu kukimbia makazi yao na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaotokana kwa kiasi kikubwa na uhalifu wa kivita.

Dk Nchimbi alisema Tanzania kama nchi muasisi wa ICGLR, imehusika na jitihada za kukomesha migogoro ndani ya kanda ikiwa ni pamoja na kuchangia vikosi vya kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Pia, alisema hivi karibuni Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa pamoja wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika Mashariki (EAC) uliolenga kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa Mashariki mwa DRC.

Dk Nchimbi amepongeza jitahada zinazoendelea katika kutafuta ufumbuzi wa migogoro katika nchi za ICGLR.

Jitihada hizo ni pamoja na zinazoongozwa na Rais wa Angola, João Lourenço za kutafuta amani DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati; Kusainiwa kwa Mkataba wa amani nchini Qatar, kuunganishwa kwa michakato ya Luanda na Nairobi na mkataba wa amani kati ya Rwanda na DRC uliosainiwa chini ya usimamizi wa Serikali ya Marekani.

Dk Nchimbi alisema licha ya jitihada hizo, bado kuna changamoto za kiusalama katika nchi mbalimbali
hususani DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Sudan.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button