Aweso ahimiza matokeo Sekta ya Maji

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewataka watumishi wa Sekta ya Maji nchini kuthibitisha imani ya Rais wa Dk Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wenye matokeo.

Aweso ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao na mapokezi yake pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Matthew mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Maji, Mji wa Serikali Mtumba.

“Tuzingatie hotuba ya Rais Samia kwa Sekta ya Maji kwa kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yetu ili kuhakikisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira zinawafikia wananchi wote kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili,” amesema Aweso.

Amewataka watumishi wote kushikamana, kufanya kazi kwa uadilifu na kasi kwa sababu Sekta ya Maji inagusa uhai wa kila Mtanzania, hivyo utekelezaji wa miradi ya maji ni lazima uende kwa kasi na ubora.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Matthew amewataka watumishi kuthibitisha takwimu za maandiko na uhalisia, kuhakikisha mafanikio ya sekta yanapimika na kuonekana, akisisitiza umuhimu wa kupunguza malalamiko ya wananchi kwa kutoa huduma bora na kuwafikia kwa wakati.

“Mafanikio tunayoyatafuta hayatakuja kwa bahati. Yatatokana na kujituma katika kazi, nidhamu, mipango mizuri na usimamizi makini wa rasilimali,” amesema Mhandisi Kundo.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amewapongeza Waziri Aweso na Naibu Waziri Kundo kwa kuendelea kuonesha umahiri wa uongozi na kujitoa kwao katika kuboresha Sekta ya Maji.

Aidha, amewahakikishia kuwa Menejimenti na Watumishi wote wa Sekta ya Maji kuungana nao katika utekelezaji wa majukumu, kusimamia Sera na Malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Habari Zifananazo

15 Comments

    1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website

    More Details For Us→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button