Diwani Manara aanza na kasi Kariakoo

DAR ES SALAAM: DIWANI mpya wa Kata ya Kariakoo, Haji Manara, ameishukuru jamii ya Kariakoo kwa kujitokeza kwa wingi na kumpa ushindi mkubwa wa asilimia 98 katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiahidi kutoa kipaumbele kwa usafi na maboresho ya miundombinu katika kitovu hicho cha biashara nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Manara alisema idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura inaonesha imani waliyonayo kwake na kwamba atahakikisha anasimamia ahadi alizozitoa mara baada ya kuapishwa.
“Niwashukuru wapiga kura wa Kariakoo. Uchaguzi wote ni mgumu, lakini nimeshinda vizuri kwa asilimia 98. Watu walijitokeza kwa wingi na hilo limenipa nguvu kubwa ya kutimiza wajibu wangu,” amesema.
Manara alisema Kariakoo ni kitovu cha biashara nchini na kinachangia mabilioni ya fedha katika Halmashauri ya Ilala kila mwaka, hivyo haiwezekani eneo hilo muhimu liendelee kukabiliwa na changamoto za miundombinu duni, hasa mitaro, chemba na maji machafu.

Amesema licha ya Kariakoo kuzalisha mapato makubwa, bado inakabiliwa na uchafu na mifereji isiyopitika, jambo linalowapa wakati mgumu wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Manara amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga Wizara maalum ya vijana kusaidia maendeleo ya vijana akisema tangu nchi ipate uhuru haijawahi kutokea tena akaiweka ofisini kwake.
Pia, aliwahimiza vijana wamsaidie Rais Samia kwa fikra na maono mazuri.




Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting websiteMore Details For Us→→ http://www.job40.media