Waziri Ndejembi akabidhiwa ofisi

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi leo Novemba 20, 2025, amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko kwenye ofisi za Wizara zilizoko Mtumba mkoani Dodoma, na kumshukuru Dk Biteko kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote cha uongozi wake.

Waziri Ndejembi amesema katika kipindi cha uongozi wake, utendaji kwenye sekta ya nishati umekua kwa kiasi kikubwa na huduma za utendaji zimeboreshwa na tija kuonekana katika harakati za kukuza sekta ya nishati.

SOMA: Lesotho wavutiwa sekta ya nishati Tanzania

Ameahidi atayaendeleza yote pale alipoishia Dk Biteko, ili kuhakikisha azma ya serikali na maono iliyonayo kufanikisha miradi ifikapo 2030 yanafikiwa.

Kwa upande wake,Dk Biteko amempongeza Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na kumhakikishia kumpa ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Nishati.

“Mengi niliyojifunza kipindi nikiwa Wizara ya Nishati lakini jambo kubwa zaidi ni sala zangu kwenu katika utekelezaji wa kazi zenu za kila siku, “ amesema Biteko.

Halfla ya makabidhiano hayo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button