Shirika la kimataifa kuendeleza ushirikiano miradi na Tanzania

SHIRIKA la Maendeleo ya Mfuko wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNDCF) limekubali kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza Programu ya LoCAL awamu ya pili. Kupitia programu hiyo, serikali inatekeleza Mradi wa Uhimili na Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi wa Dola za Marekani milioni 11 katika halmashauri 18 Tanzania Bara na Zanzibar.

Hayo yamejiri katika Mkutano wa Uwili kati ya Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Mitawi na Ofisa kutoka Shirika la UNCDF, Damiano Borgogno pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) unaoendelea jijini Belem, Brazil ambapo Tanzania inashiriki.

Katika mazungumzo yao, pia Shirika la UNCDF limeonesha nia ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika maeneo mengine yanahusiana na hifadhi endelevu ya mazingira. Amesema serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wadau wa maendeleo nchini, lengo ni kuhakikisha nchi inapata miradi zaidi na hivyo kuifanya Tanzania kuwa ni nchi yenye maendeleo endelevu katika eneo la mazingira.

SOMA: Kampeni yazinduliwa kuimarisha uchumi wa buluu Afrika Mashariki

Eneo mojawapo la ushirikiano lililotajwa ni la Uchumi wa Buluu ambalo ni sekta muhimu inayokua kwa kasi na kuchochea uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla endapo rasilimali zake zitatumiwa ipasavyo. Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imeanzisha Kitengo maalumu cha kuratibu Uchumi wa Buluu na inaendelea kuratibu na kutekeleza Sera ya Uchumi wa Buluu na Mkakati wake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button