‘Matokeo tafiti yalete majawabu ya kisayansi kwa wananchi’

Watafiti nchini wametakiwa kuhakikisha matokeo ya tafiti zinazofanywa zinaleta majawabu ya kisayansi kwa wananchi hususan katika kupunguza uharibifu wa ardhi au udongo kwa kurejesha ardhi iliyoharibika.

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe ametoa wito huo alipomwakilisha Katibu Mkuu, Mhandisi Cyprian Luhemeja katika Maadhimisho ya Siku ya Udongo Duniani Kitaifa katika Viwanja vya Nane Nane jijini Dodoma leo Desemba 03, 2025.

Prof. Msoffe amesema kuwa ili kuleta tija katika sekta ya kilimo nchini, watafiti hao wanapaswa kuhamasisha wakulima na wananchi kwa ujumla njia bora za kilimo zinazolinda udongo na mazingira kwa ujumla.

Akiwasilisha mada katika mjadala wakati wa maadhimisho hayo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ina dhamana ya Uratibu na Usimamizi wa Mazingira nchini itaendelea kuandaa Sera, Sheria, Kanuni, Mikakati na Programu madhubuti zinazolenga kuhakikisha mazingira yanakuwa salama.

Naibu Katibu Mkuu Prof. Msoffe amesisitiza kuwa afya ya udongo ni muhimu katika utunzaji wa mazingira hivyo hauwezi kuzungumzia uhifadhi wa mazingira bila kuzungumzia afya ya udongo.

Hivyo, amepongeza jitihada zilizofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika kuhakikisha kuwa masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira yanajumuishwa katika mjadala huo muhimu.

Maadhimisho hayo kwa mwaka 2025 yameandaliwa na TARI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakichagizwa na Kaulimbiu isemayo ‘Afya Bora ya Udongo kwa Majiji Maridhawa’.

Vilevile, katika kuhakikisha Maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Afya ya Udongo, yameambatana na Mjadala (Panel discussion).

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button