Makalla akagua ujenzi barabara Arusha

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla leo Jumatano Desemba 03, 2025 amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini – Timbolo – Olemringaringa- Ngaramtoni – Hospitali ya Selian yenye urefu wa Km 18, inayojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh bilioni 23.
Mara baada ya ukaguzi huo, Makalla amemsisitiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo STECOL Corporation kuongeza kasi ya kufanya kazi na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kulingana na mkataba, kwa kuwa serikali imeshalipa fedha zote za utekelezaji wa mradi huo utakaoongeza mtandao wa barabara mkoani Arusha.

Aidha, amemshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Sh bilioni 3.5 kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara hiyo, changamoto ambayo imechangia ukamilishaji wa mradi huo.
“Kulikuwa na changamoto ya madai ya fidia lakini sasa wanachi wameshalipwa fedha zao, hivyo kazi iliyobaki ni mkandarasi kukamilisha barabara hii ambayo ni muhimu kwa kiwahudumia wakazi wa Arumeru Magharibi,”amesema CPA Makalla.
Naye, msimamizi wa mradi huo, Yuan Rui wa Kampuni ya STECOL na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Dk Johannes Lukumay wameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa mradi huo, Rui akiahidi kuhakikisha kuwa barabara hiyo inakamilika kulingana na mkataba, akisema mradi huo pia utaondoa adha ya mafuriko kwenye makazi ya watu.

Ameongeza kuwa BOT itaendelea kuhakikisha mifumo ya malipo nchini inakuwa salama, ikiwemo kuimarisha usimamizi wa usalama mtandao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. (CPA) Sylvia Temu, amesema makubaliano hayo yataongeza uwazi na kuaminika kwa taarifa za kifedha zinazotolewa na wakaguzi na wahasibu waliorejistishwa na bodi hiyo.
“Mkataba huu utatusaidia kuhakikisha taarifa zote za ukaguzi zinazowasilishwa NBAA kimtandao zinakuwa na credibility ya juu, zinatumika na wadau kama benki, TRA na wawekezaji bila kubabaisha. Hii itaongeza thamani na uaminifu katika tasnia yetu,” amesema Prof. Temu.

Amebainisha pia kuwa maendeleo ya teknolojia na viwango vipya vya uandaaji wa hesabu vinavyolenga uendelevu (sustainability reporting) vitahitaji wahasibu kuwa na ujuzi wa ziada na kuendelea kuzingatia maadili, ili kuendana na matarajio ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania katika miaka 25 ijayo.
Mshiriki wa mkutano huo, ACPA Magdalena Osima, ambaye ni Meneja Mkuu wa Halisi Microfinance Limited, amesema ameona makubaliano kati ya BOT na NBAA kama hatua muhimu itakayowezesha taasisi mbalimbali kupata taarifa za kifedha kwa urahisi zaidi kupitia teknolojia. Amesema matumizi ya mifumo ya kisasa yataongeza ufanisi na kusaidia taasisi kunufaika na taarifa sahihi, hivyo kuongeza uwezo wa kufanya maamuzi bora katika sekta ya fedha.
Mkataba huo unatarajiwa kuimarisha uandaaji wa taarifa za kifedha kwa kutumia mifumo ya kidijitali, kurahisisha upatikanaji wa data, na kuongeza ushirikiano kati ya wadau wakuu wa uchumi.




Epuka kujiunga au kushiriki kwenye makundi ya mtandaoni yanayochochea vurugu. Ni kosa kwa mujibu wa sharia.