Mwakagenda Mwenyekiti mpya Halmashauri Rungwe

MBEYA; MADIWANI katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wamemchagua Gabriel Mwakagenda kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Katika Kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo Mwakagenda amechaguliwa kwa kupata kura za ndiyo zote 42 zilizopigwa.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa Mwakagenda ameahidi ushirikiano kwa madiwani wote akiwemo Diwani wa Kata ya Makandana wa Chama cha ACT-Wazalendo akisema kitendo cha yeye kuungana na madiwani wa CCM kunamaanisha ana lengo la kuwa na umoja katika kuwaletea maendeleo wananchi.



