Mzumbe yataka matukio ya Oktoba 29 yawe darasa

CHUO Kikuu cha Mzumbe kimewataka wahitimu wake wajifunze kwa yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu. Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Profesa Saida Yahya- Othman amesema  hayo kwenye Mahafali ya 24 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam.

Profesa Saida amesema moja ya mambo yanayostahili kuwa darasa kwa wahitimu hao ni matukio ya vurugu katika siku hizo. “Nchi yetu mambo ambayo imepitia hivi karibuni nayo yanakuwa sehemu ya darasa letu la dunia la uvumilivu kwa pande zote, darasa la uvumilivu, usikivu na ufahamu na ubunifu. Msilisahau darasa hili, mjifunze katika kuchangia mabadiliko na maendeleo ya jamii,” alisema Profesa Saida.

Profesa Saida amewatahadharisha wahitimu hao kutumia vizuri mitandao ya kijamii katika kutafuta maendeleo na kujenga badala ya kuitumia kubomoa. “Usemi wa elimu haina mwisho…usemi huu haugusi elimu za shuleni tu au vyuoni tu, maisha yetu yote tumekuwa tunasaka majibu na maarifa juu ya mambo anuai na majibu hayo tunayapata kutoka dunia yote inayotuzunguka ya karibu na ya mbali,” alieleza.

Amesema dunia ni darasa na maarifa yake ni ya muhimu hata yakitoka kwa wale ambao hawajaingia darasani. “Najua vijana mpo kwenye mitandao sana na sasa hivi kwenye mitandao kuna vitu vinaweza kukusaidia kufanya jambo kwa wepesi ambavyo kabla ya hapo tulikuwa tunachukua muda kuvifanya… kwa hiyo mambo hayo hayatoki kwa watu waliokuwa darasani,” alisema. SOMA: Mapingamizi yasimamisha uchaguzi wa mwenyekiti Chato

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button