ADA-TADEA kuifanya Tanzania ya teknolojia

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha African Democratic Alliance (ADA-TADEA, George Busungu amesema serikali yake itawapa kipaumbele wabunifu wa ndani kwa kujenga mji wa teknolojia ili kuchangia kukuza uchumi.

Basungu alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Malampaka wilayani Maswa mkoani Simiyu juzi. “Tunataka kuifanya Tanzania iwe nchi ya ubunifu, tutajenga mji maalumu wa teknolojia ambapo vijana wabunifu watapata nafasi ya kufanyia kazi mawazo yao, kuzalisha bidhaa hapa nchini badala ya kuagiza nje. Hii ndiyo njia ya kuinua uchumi wa taifa letu,” alisema.

Busungu alisema sera ya chama hicho inalenga kujenga misingi ya uchumi wa kisasa, unaotegemea maarifa na ubunifu sanjari na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi kushiriki katika maendeleo. Kwa upande wake, Katibu wa Uenezi wa chama hicho, Salehe Mohamed alisema sera za ADA-TADEA zimetilia mkazo kuboresha maisha ya kila Mtanzania.

“Tumeandaa sera zinazogusa maisha ya kila Mtanzania. Watumishi wa afya, walimu na askari polisi watapewa motisha na mazingira bora ya kazi ili kutoa huduma zenye tija kwa wananchi,” alisema Mohamed. SOMA: Teknolojia kuimarisha uchumi Bara, Zanzibar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button