TAASISI isiyokuwa ya kiserikali inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya sanaa na utamaduni (ADEA) Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imeendelea kutoa mafunzo kwa mafundi selemala ili kuwaongezea ujuzi wa sanaa katika kazi zao hizo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ya (ADEA) Saidi Chilumba amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa kutoa elimu kwa vijana kwa kwenye makundi mbalimbali hasa ya ufundi stadi kipitia ujuzi na sanaa.
Mafunzo hayo lenye lengo la kuwapa ujuzi vijana hasa waliopo ndani ya manispaa hiyo wa kuboresha kazi zao wanazozifanya kila siku na zinahitaji zaidi ubunifu.
“Dunia inavyokwenda inahitaji ubunifu tusipofanya hivyo vijana walio wengi watakosa fursa za baadae, dunia inavyokwenda inahitaji watu wenye ubunifu, tumeona eneo hilo lina changamoto tumeamua kuwapa fursa vijana hasa eneo la useremala, uchongaji, fundi chuma na uchoraji,”amesema Chilumba.
Amewataka vijana hao kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa bure kwa ajili ya kukuza vipaji vyao na kuongeza ubunifu ili waweze kutambulika kitaifa na dunia kwa ujumla.
Sharifu Mapila muwezeshaji katika mafunzo hayo, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana kwasababu kupitia mafunzo vijana wanapata nafasi ya kujitangaza kitaifa kwa kupata ajira sehemu tofauti tofauti.
Abdul Rashid ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo ameelezea matarajio yake baada ya mafunzo hayo kuwa ni namna ya kuongezea kazi zao thamani na kuzidisha umakini sehemu zao za kazi.
Mafunzo hayo yanatolewa na taasisi hiyo ya ADEA ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya kuimarisha sanaa, utamaduni, na ufundi stadi kwa vijana mafunzo hayo.
Mafunzo ambayo yanafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (UNESCO) ambpo yanatarajiwa kunufaisha mafundi seremala 24 kutoka kwenye manispaa hiyo