AFINet kuendeleza wachimbaji wadogo

GEITA: MTANDAO wa Wawekezaji Kwanza Afrika (AFINet) imepanga kufanya mtoko wa kitaifa ili kutambulisha na kuendeleza wachimbaji wadogo nchini na kuwafanya wakidhi mahitaji ya teknolojia, utalaamu na raslimali.

Katibu wa AFINet, Edmund Kaiza ametoa taarifa hiyo mbele ya wanaandishi wa habari katika viwanja vya Dk Samia Suluhu Hassan yanapofanyika Maonyesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Amesema dhamira ya mtoko huo pia ni kuhusianisha ujuzi na soko la ajira kupitia tafiti na utalaamu elekezi, hususani katika sekta ya uchimbaji, uchakataji, uchenjuaji na uchuuzi wa madini na uongezaji thamani.

Kaiza amesema mtoko utaendeshwa nchi nzima kila mkoa kwa kushirikisha kampuni za watalaamu, wachimbaji wadogo na wananchi waliojumuika kuunda AFINet .

“Katika kuhakikisha kuwa lengo kuu linafikiwa Jukwaa la Mtandao wa Wawekezaji Kwanza litafanyika siku tatu kila mkoa ambapo mtoko utaendeshwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa Magharibi” amesema.

Amesema mtoko huo unakusudia kutoa mchango mkubwa katika uendelezaji wa sekta ya madini kama nguzo muhimu ya kujumuisha wananchi wote kuwa wabia wa serikali wanaoshiriki kikamilifu kujenga na kumiliki uchumi nchi.

“Aidha mtoko huu utachangia ipasavyo kutatua vhangamoto kubwa ya kuziba pengo lililopo kati ya taaluma wanazopata vijana vyuoni na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira hususani kwenye sekta ya madini na viwanda”, amesema Kaiza.

Mwakilishi wa Kansel Gold Mine.Co.Ltd, Regina Kabogo amesema jukwaa la AFINet linatarajia kkuongeza uwingi wa upatikanaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo nakuwapa fursa kubwa ya kutawala sekta ya madini.

Amesema matarajio ni kuona kila mtanzania mwenye uwezo na dhamira ya kuwekeza kwenye sekta ya madini anafanikiwa kikamirifu pasipo kuwa na kikwazo ili kuwafanya wazawa kuwa vinara wa uwekezaji nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button